Nenda kwa yaliyomo

Ukambi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Surua)
Ukambi
Mwainisho na taarifa za nje
SpecialtyInfectious diseases Edit this on Wikidata
ICD-10B05.
ICD-9055
DiseasesDB7890
MedlinePlus001569
eMedicinederm/259 emerg/389 ped/1388
MeSHD008457

Ukambi (au surua) ni ugonjwa wa kuambukiza unaoenezwa sana kupitia mgusano yanayosababishwa na virusi vya ukambi.[1][2]

Ishara na dalili za kwanza kwa kawaida hujumuisha homa, ambayo mara nyingi huwa zaidi ya °C 40 (°F 104.0), kikohozi, mafua, na macho mekundu.[1][3] Siku mbili au tatu baada ya dalili kuanza, madoa madogo meupe yanaweza kuonekana ndani ya kinywa yanayojulikana kama alama za koplik. Chunusi nyekundu, zinazoanza kwenye uso kisha kuenea kwa mwili wote, kwa kawaida huanza siku tatu hadi tano baada ya mwanzo wa dalili.[3]

Dalili kwa kawaida huwa siku 10–12 baada ya kutangamana na mtu aliyeambukizwa kwa siku 7–10.[4][5]

Matatizo zaidi ya ukambi hutokea kwa takriban asilimia 30 na yanaweza kujumuisha kuhara, upofu, inflamesheni ya ubongo, na nimonia miongoni mwa mengine.[4][6]

Rubela na roseola ni magonjwa tofauti ingawa yanafanana na surua.[7]

Kisababishi na utambuzi[hariri | hariri chanzo]

Ukambi ni ugonjwa unaoambukiza kupitia hewa na kuenezwa kwa urahisi na watu walioambukizwa kupitia kikohozi na kupiga chafya. Pia unaweza kuenezwa kupitia kutangamana na mate au makamasi.[4] Watu tisa kati ya kumi wasio na kingamwili wanaokaa pamoja na mtu aliyeambukizwa wataambukizwa ukambi. Watu huweza kuwaambukiza wengine katika siku nne kabla hadi siku nne baada ya mwanzo wa chunusi.[6]

Watu kwa kawaida hupata ugonjwa huu mara moja tu.[4] Vipimo vya virusi hivi katika visa vinavyokisiwa ni muhimu kama sehemu ya juhudi za afya ya umma.[6]

Kinga na tiba[hariri | hariri chanzo]

Chanjo ya ukambi huwa mwafaka katika kuzuia ugonjwa huu. Uchanjaji umepunguza asilimia 75 ya vifo vilivyotokana na ukambi kati ya miaka ya 2000 na 2013 na takriban asilimia 85 ya watoto ulimwenguni kote wanapata chanjo kwa sasa.

Hakuna matibabu maalum ya ukambi. Hata hivyo, utunzaji wa kimsaada unaweza kuboresha matokeo.[4] Hii inaweza kujumuisha kuwapa wagonjwa mmumunyo wa chumvi-maji za kunywa (viowevu vyenye utamu na chumvi), vyakula vyenye afya na dawa ya kupunguza homa.[4][5] Antibiotiki zinaweza kutumika ikiwa maambukizi ya bakteria kama vile ya numonia yatatokea. Nyongeza ya Vitamini A hupendekezwa katika nchi zinazoendelea.[4]

Epidemiolojia na prognosisi[hariri | hariri chanzo]

Ukambi huathiri takriban watu milioni 20 kila mwaka,[1] hasa katika maeneo yanayoendelea barani Afrika na Asia.[4] Ukambi husababisha vifo vingi vinavyoweza kuzuiwa kwa kutumia chanjo ikilinganishwa na magonjwa mengine.[8] Ukambi ulisababisha takriban vifo 96,000 katika mwaka wa 2013 ikilinganishwa na vifo 545,000 katika mwaka wa 1990.[9] Katika mwaka wa 1980, ugonjwa huu ulikadiriwa kusababisha vifo milioni 2.6 kila mwaka.[4] Kabla ya uchanjaji nchini Marekani, kati ya visa milioni tatu na milioni nne vilitokea kila mwaka.[6] Watu wengi wanaoambukizwa na kufariki huwa wenye umri wa chini ya miaka mitano.[4] Hatari ya kifo kwa walioambukizwa kwa kawaida huwa asilimia 0.2,[6] lakini hii inaweza kuongezeka hadi asilimia 10 kwa wale walio na utapiamlo.[4] Ukambi hauaminiki kuathiri wanyama.[4]

Marejeleo[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 1.2 Caserta, MT, mhr. (Septemba 2013). "Measles". Merck Manual Professional. Merck Sharp & Dohme Corp. Iliwekwa mnamo 23 Machi 2014.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "Measles (Red Measles, Rubeola)". http://www.health.gov.sk.ca/. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-02-10. Iliwekwa mnamo 10 Februari 2015. {{cite web}}: External link in |website= (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. 3.0 3.1 "Measles (Rubeola) Signs and Symptoms". cdc.gov. Novemba 3, 2014. Iliwekwa mnamo 5 Februari 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. 4.00 4.01 4.02 4.03 4.04 4.05 4.06 4.07 4.08 4.09 4.10 4.11 "Measles Fact sheet N°286". who.int. Novemba 2014. Iliwekwa mnamo 4 Februari 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. 5.0 5.1 Conn's Current Therapy 2015: Expert Consult - Online. Elsevier Health Sciences. 2014. uk. 153. ISBN 9780323319560.
  6. 6.0 6.1 6.2 6.3 6.4 Atkinson, William (2011). Epidemiology and Prevention of Vaccine-Preventable Diseases (toleo la 12). Public Health Foundation. ku. 301–323. ISBN 9780983263135. Iliwekwa mnamo 5 Februari 2015.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  7. Marx, John A. (2010). Rosen's emergency medicine : concepts and clinical practice (toleo la 7th ed.). Philadelphia: Mosby/Elsevier. uk. 1541. ISBN 9780323054720. {{cite book}}: |edition= has extra text (help)
  8. Kabra, SK; Lodhra, R (14 Agosti 2013). "Antibiotics for preventing complications in children with measles". Cochrane Database of Systematic Reviews. 8: CD001477. doi:10.1002/14651858.CD001477.pub4. PMID 23943263.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  9. GBD 2013 Mortality and Causes of Death, Collaborators (17 Desemba 2014). "Global, regional, and national age-sex specific all-cause and cause-specific mortality for 240 causes of death, 1990-2013: a systematic analysis for the Global Burden of Disease Study 2013". Lancet. doi:10.1016/S0140-6736(14)61682-2. PMID 25530442. {{cite journal}}: |first1= has generic name (help)CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: numeric names: authors list (link)