Nenda kwa yaliyomo

Chanjo ya ukambi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Chanjo ya ukambi
Vaccine description
Target disease Measles
Type Attenuated virus
Clinical data
MedlinePlus a601176
Pregnancy cat. ?
Legal status ?
Identifiers
ATC code J07BD01
ChemSpider NAKigezo:Chemspidercite
 N(what is this?)  (verify)

Chanjo ya ukambi ni chanjo bora sana ambayo hujenga kinga madhubuti dhidi ya surua.[1] Baada ya kupata dozi moja, asilimia 85 ya watoto wa umri wa miezi tisa na asilimia 95 ya walio zaidi ya miezi kumi na miwili hupata kingamwili.[2] Takriban watoto wote wasiopata kingamwili baada ya dozi moja hupata kingamwili hii baada ya dozi ya pili. Kiasi cha uchanjaji katika idadi jumla ya watu ikiwa zaidi ya asilimia 93, milipuko ya ukambi kwa kawaida haitokei tena; hata hivyo inaweza kutokea tena ikiwa kiasi cha uchanjaji kitapunguka. Ubora wa chanjo hii huwepo kwa miaka mingi. Haijulikani ikiwa ubora huu hupunguka baada ya miaka kadhaa. Chanjo hii pia inaweza kukinga dhidi ya ugonjwa huu ikiwa katika siku chache umetangamana na ugonjwa huu.[1]

Chanjo hii ni salama kwa ujumla ikijumuisha hata walio na maambukizi ya VVU. Athari kwa kawaida huwa si kali na ni za muda mfupi. Hii inaweza kujumuisha maumivu katika sehemu ya mwili iliyodungwa au homa kiasi. Anafilaksisi imenakiliwa kwa takriban mtu mmoja kwa kila watu elfu mia moja. Kiasi cha Sindromu ya Guillian-Barre, otizimu na ugonjwa wa inflamesheni ya utumbo hakionekani kuongezeka.[1]

Chanjo hii inapatikana kivyake au katika mchanganyiko na chanjo zingine ikijumuisha chanjo ya rubela, chanjo ya matubwitubwi, na chanjo ya tetekuwanga ( chanjo ya Ukambi, Matubwitubwi na Rubela and chanjo ya Ukambi, Matubwitubwi, Rubela na Tetekuwanga). Chanjo hii hufanya kazi vyema hata katika miundo yote. Shirika la Afya Duniani hupendekeza kuwa chanjo hii itolewe kwa watoto katika umri wa miezi tisa katika maeneo ya ulimwengu ambapo ugonjwa huu hutokea mara nyingi. Katika maeneo ambayo ugonjwa huu hautokei mara nyingi, kutoa chanjo hii katika umri wa miezi kumi na miwili inafaa. Hii ni chanjo ya maishani. Chanjo hii huwa katika aina ya poda iliyokaushwa inayohitaji kuchanganywa kabla ya mtoto kudungwa chini ya ngozi au katika misuli. Uthibitishaji kuwa chanjo hii ni bora unaweza kutambuliwa na vipimo vya damu.[1]

Takriban asilimia 85 ya watoto ulimwenguni kote wamepata chanjo hii kuanzia mwaka wa 2013.[3] Katika mwaka wa 2008, angalau nchi 192 zilitoa dozi mbili za chanjo hii.[1] Chanjo hii ilianzishwa kwa mara ya kwanza katika mwaka wa 1963.[2] Mkusanyiko wa chanjo ya ukambi-matubwitubwi-na rubela ilipatikana kwa mara ya kwanza katika mwaka wa 1971.[4] Chanjo ya tetekuwanga iliongezwa kwa mkusanyiko huu katika mwaka wa 2005 hivyo kutengeneza chanjo ya Ukambi, Matubwitubwi, Rubella na Tetekuwanga.[5] Chanjo hii ipo katika Orodha ya Shirika la Afya Ulimwenguni ya Dawa Muhimu, dawa muhimu zaidi inayohitajika katika mfumo wa afyawa kimsingi.[6] Chanjo hii haina gharama ya juu sana.[1]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 "Measles vaccines: WHO position paper" (PDF). Weekly epidemiological record. 84 (35): 349–60. 28 Agosti 2009. PMID 19714924.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.0 2.1 Control, Centers for Disease; Prevention (2014). CDC health information for international travel 2014 the yellow book. uk. 250. ISBN 9780199948505.
  3. "Measles Fact sheet N°286". who.int. Novemba 2014. Iliwekwa mnamo 4 Februari 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. "Vaccine Timeline". Iliwekwa mnamo 10 Februari 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. Mitchell, Deborah (2013). The essential guide to children's vaccines. New York: St. Martin's Press. uk. 127. ISBN 9781466827509.
  6. "WHO Model List of EssentialMedicines" (PDF). World Health Organization. Oktoba 2013. Iliwekwa mnamo 22 Aprili 2014.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Chanjo ya ukambi kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.