Nenda kwa yaliyomo

Mali kwa mali

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Uchoraji wa mwaka 1876 unamwonyesha mkulima Mmarekani anayejaribu kulipa deni dukani kwa kuku; uso wa mwenye duka unaonyesha wakati ule haikuwa njia ya kawaida
Mnamo 1769 Maori alimpa baharia Mwingereza samaki wa kamba akipata kipande cha nguo (uchoraji kutoka New Zealand)

Mali kwa mali (kwa Kiingereza: barter) ni biashara ya kubadilishana bidhaa kwa bidhaa bila kutumia hela. [1] Kawaida bidhaa zinazobadilishwa zinatakiwa kuwa na thamani sawa. Umbo tofauti la biashari hii ni kulipa kwa bidhaa, yaani kubadilisha huduma kwa bidhaa.

Mali kwa mali ilikuwa njia ya kawaida ya biashara baina ya jamii tofauti kabla ya kusambaa kwa hela. Katika jamii za kisasa si kawaida, isipokuwa katika mazingira ambapo thamani ya pesa imeshuka mno, yaani hali ya mfumukobei mkali.

Biashara ya mali kwa mali inafaa kama watu wawili ambao wana vitu ambavyo vinahitajiwa na mwingine. Ilitokea hasa katika mazingira ya vijijini ambako mazao mbalimbali na bidhaa zilizotengenezwa na wahunzi au wafinyanzi zinaweza kubadilishwa. Ilikuwa kawaida katika Afrika ya Mashariki wakati wa biashara ya misafara hadi karne ya 19 ambako vitu kutoka nje kama vitambaa, ushanga (gololi za kioo), waya, silaha za moto au pombe kali zilibadilishwa kwa pembe za ndovu au watumwa.[2]

Katika mazingira ya biashara ya kubadilishana vinaweza kutokea vitu kadhaa vinavyofanya kazi kama pesa. Mara nyingi ni mifugo; katika Kenya kwenye mwanzo wa karne ya 20 ilikuwa kawaida kukadiria ng'ombe 1 sawa na kondoo au mbuzi 10; viwango hivyo vilikuwa kawaida hadi miaka ya 1930 hivi, pamoja na ushanga (uliitwa "ukuta" pale) na kombe za kauri kwa manunuzi madogo[3].

  1. "Barter". Merriam-Webster Dictionary. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-10-12. Iliwekwa mnamo 01-06-2007. {{cite web}}: Check date values in: |accessdate= (help)
  2. "Traditional barter market". TradeMark East Africa. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-02-01. Iliwekwa mnamo 01-02-2020. {{cite web}}: Check date values in: |accessdate= (help)
  3. Claire Cone Robertson: Trouble Showed the Way: Women, Men, and Trade in the Nairobi Area, 1890 - 1990; Indiana University Press 1997, ISBN 978-0253333605; online hapa
Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mali kwa mali kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.