Gololi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Gololi ni kitufe cha glasi, kigae au marumaru ambacho kinatumika katika aina fulani ya michezo ya watoto Afrika Mashariki na kwingineko.

Pia ni kitufe cha chuma kinachowekwa kwenye belingi ya baiskeli na vyombo vingine vya usafiri.

Tena ni kiwambo cheupe ndani ya jicho kinachosababisha upofu.

Hatimaye neno hilo linatumika kwa korodani au kende ya mwanamume au mnyama dume.