Nenda kwa yaliyomo

Magugu (Babati)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Magugu ni kata ya Wilaya ya Babati Vijijini katika Mkoa wa Manyara, Tanzania yenye postikodi namba 27201.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 43,282 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 32,774 waishio humo.[2]

Kata ya Magugu ina wakazi wa makabila mbalimbali, ila watu wa asili wa kata hii ni kabila dogo la Wambugwe. Wengine ni hasa Wairaqw, Warangi, Wanyaturu, Wanyiramba na makabila mengine madogomadogo.

Wakazi walio wengi wanajihusisha na kilimo cha mazao mbalimbali ya chakula na biashara, hasa mpunga, karanga, mtama, miwa, alizeti pamoja na ufuta.

Katika uwanja wa elimu kata ya Magugu ina shule kadhaa za serikali na za binafsi zinazotoa elimu kwa ngazi ya msingi na ya sekondari. Shule hizo ni: Shule ya msingi Magugu, Shule ya msingi Kibaoni, Shule ya msingi Mekiroy, Shule ya msingi Joshua, Shule ya msingi Glory Junior, Shule ya Holy Land, Shule ya msingi Mapea, Shule ya msingi Gichameda, halafu Shule ya sekondari Magugu, Shule ya sekondari Joshua, Shule ya sekondari Holy land, Shule ya sekondari Matufa na Shule ya sekondari Gichameda.

Shule ya sekondari Magugu iliyoanza mwaka 2005 ina takribani wanafunzi 900 na walimu takribani 43, lakini walimu 6 hivi ni wa masomo ya sayansi na baadhi yao ni wakongwe wa shule hiyo (Dominick Medard, Msungu Henry, Laurence Manimo, Pareso Richard, Gerny Shigela na Fiita Sandemu). Mkuu wa shule wa kwanza ni Mwl. Magambo akafuatiwa na Mwl. Maginga na wa sasa anaitwa Mfwangavo.

Kata za Wilaya ya Babati Vijijini - Mkoa wa Manyara - Tanzania

Arri | Ayalagaya | Ayasanda | Bashnet | Boay | Dabil | Dareda | Duru | Endakiso | Gallapo | Gidas | Kiru | Kisangaji | Madunga | Magara | Magugu | Mamire | Mwada | Nar | Nkaiti | Qameyu | Qash | Riroda | Secheda | Ufana


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Manyara bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Magugu (Babati) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.