Macbeth

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Picha ya tamthilia ya Macbeth.

Macbeth ni tamthilia ya William Shakespeare inayohusu mauaji ya mfalme na athari yake. Ni tamthiliya fupi kabisa ya Shakespeare inayoaminika kuandikwa katika miaka kati ya 1603 na 1607.

Wahusika[hariri | hariri chanzo]

  • Ross, Lennox, Angus, Menteith, Caithness - Viongozi
  • Siward - Kiongozi wa Northumberland, Mkuu wa majeshi ya Kiingereza
    • Young Siward - mtoto wa Siward
  • Seyton - mtumishi wa Macbeth
  • Hecate - Mchawi Mkuu
  • Witches - Wachawi wengine
  • Porter - Askari anayechunga nyumba ya Macbeth
  • Scottish Doctor - daktari wa Lady Macbeth
  • The Gentlewoman - mfanyikazi

Kuhusu tamthilia hii[hariri | hariri chanzo]

Macbeth pindi anapokumbana na wachawi

Tamthilia hii inaanza pindi wachawi watatu wanapokutana kujadiliana siku ambayo wataonana na Macbeth. Kuna radi na umeme. Baadaye, jeshi la Macbeth limeshinda vita dhidi ya jeshi la Norway. Macbeth, ambaye ni mkuu wa jeshi, anasifiwa kwa kazi yake.

Baadaye, Macbeth na Banquo wanakutana na wachawi watatu wanaomwambia Macbeth kuwa atakuwa kiongozi wa "Glamis" na wa "Cawdor" halafu baadaye atakuwa Mfalme. Baada ya muda kidogo tu, Ross, ambaye ni mtumwa wa Mfalme, anakuja kwa Macbeth na kumpa habari kuwa ametuzwa kwa kuwa Kiongozi wa "Cawdor". Maneno waliyosema wachawi yalianza kuwa ni ya ukweli. Papo hapo, Macbeth anafanya tamaa na kuwa na hamu ya kuwa Mfalme.

Kisha, anamwandikia mkewe barua kumwelezea kuhusu taarifa ya wachawi. Lady Macbeth anatunga njama ya kumuua Mfalme Duncan ili mumewe aupate ufalme. Ingawa Macbeth anaogopa kumuua mfalme, Lady Macbeth anamhimiza kwa kuchokoza ujanadume wake. Macbeth anakubali njama hii.

Usiku wa ziara ya mfalme katika nyumba ya Macbeth, Macbeth unamuua Duncan. Kulingana na mpango wake, anawasingizia watumishi wa Duncan waliolala kwa kuwaekea visu vilivyotapakaa damu. Mapema asubuhi iliyofuata, Lennox, ambaye ni diwani, na Macduff, ambaye ni kiongozi wa Fife, wanawasili. Askari anawafungulia mlango na kisha Macduff anapatana na maiti ya Duncan huko ndani ya nyumba. Kwa hasira za unafiki, Macbeth anawaua walinzi kabla ya wao kujitetea. Macduff anashuku vitendo vya Macbeth, lakini hasemi kitu. Watoto wa Duncan wanakimbia nje ya nchi kwa hofu ya maisha yao. Macbeth anakuwa Mfalme wa Scotland.

Macbeth anawatuma watu wawili kuwaua Banquo na Fleance. Watu hawa wanamuua Banquo, lakini Fleance alitoroka. Baada ya muda, Macbeth hana raha kwa vitendo alivyovifanya. Macbeth anamshuku Macduff, hivyo basi anamuua mkewe Macduff na watoto wake.

Lady Macbeth anababaishwa na vitendo vya kikatili yeye na mumewe walivyofanya.. Yeye anaanza kubabaika mpaka akiwa usingizini, akiongea akisema mambo aliyoyafanya ilhali akiwa amelala.

Lady Macbeth akitembea ilhali akiwa usingizini.

Macduff anapata habari ya kuwa watu wake wameuwawa. Kila mtu sasa anajua kuwa Macbeth ni katili. Malcom anaongoza jeshi la kwenda kupigana na Macbeth. Lady Macbeth anajiua.

Katika vita, jeshi la Macbeth linashindwa. Macbeth anagundua kuwa wachawi wamempotosha. Tamthilia hii inaisha pindi Macduff anapomkata kichwa Macbeth.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]