William Shakespeare

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
William Shakespeare

William Shakespeare (Aprili 1564 - 23 Aprili 1616) alikuwa mwandishi mashuhuri nchini Uingereza.

Waingereza mara nyingi humtazama kuwa mwandishi mkuu wa lugha yao. Aliandika hasa maigizo na tamthiliya. Alifanya pia kazi ya uigizaji.

Mwandishi huyo akiwa mdogo alikuwa anapenda kusoma sana hadithi mbalimbali ambazo zilikuwa zimeandikwa kwa lugha ya Kilatini. Shakespear alisoma zaidi kazi za wanafalsafa wakongwe wa Kigiriki Aristotle na Plato, pia alipenda sana teolojia.

Maigizo yake hupangwa katika vikundi vya:

Kutokana na wingi wa kazi na mada, wataalamu wengine hawakubali ya kwamba maandiko yote yanayojulikana kama ya "Shakespear" yameandikwa na mtu yeye yule, lakini walio wengi wameridhika ya kwamba huyu Shekespear wa kihistoria mwenyewe alikuwa mwandishi wa hayo yote.

Tamthiliya zake[hariri | hariri chanzo]

Kati ya maandiko yake mashuhuri ni:

Mchezo tanzia "Julius Caesar" pamoja na tamthiliya ya kuchekesha "The Merchant of Venice" vimetafsiriwa na Mwalimu Julius Nyerere kwa lugha ya Kiswahili ("Julius Kaisari" na "Mabepari wa Venisi")

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu William Shakespeare kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.