Nenda kwa yaliyomo

The Merchant of Venice

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
The Merchant of Venice
Muziki na Jocelyn Pook
Imehaririwa na Lucia Zucchetti
Imesambazwa na Sony Pictures Classics
Imetolewa tar. 29 Desemba 2004
Ina muda wa dk. 138 minutes
Nchi Italy
Ufalme wa Muungano
Luxembourg

The Merchant of Venice ni filamu ya 2004 inayoangazia Tamthilia ya William Shakespeare ya jina hilo. Ni filamu ya kwanza yenye urefu wa maonyesho yote katika Kiingereza ya tamthilia ya Shakespeare. Matoleo mengine huwa katika videotape ambayo huwa yametengenezwa kwa televisheni. Kumekuwa na toleo la Britain la sauti la urefu wa dakika tisa kwa onyesho la hukumu mnamo 1927, likishirikisha Lewis Casson kama Shylock na Sybil Thorndike (Mkewe Casson) kama Portia.

Filamu hii inauatilia kwa karibu maneno ya tamthilia, ikikosea tu katika mishororo michache hapa na pale. Mwelekezi, Michael Radford, aliamini kuwa Shylock ndiye aliyekuwa shujaa wa pekee wa Shakespeare ambaye alikumbana na janga kutokana na makosa yake binafsi. Kwa hivyo filamu hii haionyeshi shylock kama mtu mbaya kabisa lakini kwa kiasi Fulani kama mhasiriwa wa janga. Inaanza kwa sehemu inayonyesha vile Wayahudi wanachukiwa na kudharauliwa na Wakristo mjini Venice. Moja ya maonyesho ya mwisho pia huonyesha vile kama mtu aliyegeuka kwa imani na kuwa mkristo, Shylock angetupwa nje ya mtaa wa Venice na jamii ya Wayahudi

Wahusika

[hariri | hariri chanzo]

Wahusika wakuu ni Al Pacino kama Shylock myahudi, Jeremy Irons kama Antonio mfanyibiashara, Joseph Fiennes kama Bassanio na Lynn Collins kama Portia.

Wahusika wengine ni pamoja na:

Mojawapo ya mabadiliko ya muhimu: Katika Sehemu ya III onyesho la kwanza, Tubal anamwambia Shylock kuwa kule Genoa, mtu alimwonyesha bete ambayo aliinunua kutoka kwa mtu kwa mwana wa tumbili ("showed me a ring that he had of your daughter for a monkey.") Shylock anajibu, "Thou torturest me, Tubal: It was my turquoise; I had it of Leah when I was a bachelor; I would not have given it for a wilderness of monkeys." Hakuna zaidi lisemwalo. Hata hivyo katika onyesho lililoongezwa mwishoni mwa filamu, kunaonyeshwa kwa karibu pete ikiwa kidoleni mwa Jessica, ikiashiria kuwa Shylock alikuwa ameyapapia maneno na akakata kauri mbaya.

Badiliko jingine ni kuwa mwishoni mwa filamu hatuonyeshwi kuwa Antonio anapokea habari njema ya kurudi kwa meli zake tatu na kuwa hazikuwa zimekwama.

Mapokezi na Uchambuzi

[hariri | hariri chanzo]

Wachambuzi wengi wa filamu waliisifu filamu hii hasa kwa uchambuzi wa Michael Radford na Al Pacino wa tabia ya Shylock. Pia wachambuzi wanasifu uonekanaji wa kikweli wa mitaa ya Venice kwa mwangaza hafifu, ambao ulimfanya mtayarishi kupewa pongezi na kundi la Italian National Syndicate of Film Journalists. Mnamo 2005, filamu hii ilikuwa na Royal Premiere katika uwepo wa Prince Charles na ikafuzu kwa tuzo la Best Costume Design. Mauzo yake ya kijukwaa dunia nzima yalikuwa takribani dola milioni 21.3 kwa utayarishi wa milioni 30[1]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]