Michael Radford

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Michael Radford

Amezaliwa 24 Februari 1946 (1946-02-24) (umri 78)
New Delhi, India

Michael Radford (amezaliwa 24 Februari 1946 mjini New Delhi, India) ni mtunzi wa michezo ya screen na mwongozaji wa filamu wa Uingereza. Baba'ke ni wa asili ya Uingereza na mamake ana asili ya Austria- myahudi.

Maisha ya awali na kazi[hariri | hariri chanzo]

Radford alisomea katika Shule ya Bedford kasha akajiunga na Worcester College, Oxford. Baada ya kufunza kwa miaka michache,alijiunga na National Film and Television School, ambapo alianza kuwa mwanafunzi katika mwaka wake wa kuanzishwa.

Kati ya 1976 na 1982 Radford alifanya kazi kama mtengenezaji filamu za documentary, sana sana akitunga miradi ya BBC, akiangazia maswala kama vile wakazi wa kisiwa cha Scotland cha Lewis maeneo ya nje ya the Outer Hebrides ambao wanaamini katika ukweliw wa kifasaha wa Biblia: Injili ya Mwisho; mwimba sauti ya juu sana Isobel Buchanan: 'La Belle Isobel'; mwimbaji na mtunzi Van Morrison: Van Morrison in Ireland; na makala ya 'The Making of The Pirates of Penzance'. Katika makala mawili ya mwisho, Radford alishirikiana na sinematografa Roger Deakins, ambaye baadaye alinasa filamu mbili za kuangaziwa za Radford, 1984 (filamu) na White Mischief. Pia makala ya kumakiwa katika utayarishi wake wa mwanzo ni 'Another time, another place' (1982), filamu ya kuangaziwa iliyonasiwa Scotland wakati wa Vita vya Pili vya Dunia na inajikitha katika hadithi ya mapenzi kati ya mwanamke wa nchi hiyo na Mateka wa Vita wa Italia.

Ufanisi[hariri | hariri chanzo]

Michael alifahamika duniani wakati wa filamu yake ‘’1984’’, ambayo ni fashi=oni yake ya filamu kutokana na riwaya ya George Orwell, Nineteen Eighty-Four, ambayo nyota wake ni John Hurt kama Winston Smith, na pia filamu ambapo Richard Burton aliigiza kwa mara ya mwisho. Filamu hii ilitengenezwa jijini London mnamo Aprili hadi Juni 1984, wakati na mahali ambapo riwaya hiyo ilitengenezewa.

Filamu yake iliyofuatia ilitolewa mnamo 1987 ambayo ni White Mischief, igizo la muda katika historia lililofanyiwa nchini Kenya miaka ya 1940. Radford pia aliandika tamthilia ya kuonyesha kutokana na riwaya ya Jamie Fox ambayo pia inaitwa White Mischief.

Michael Radford anajulikana kama mwelekezi wa filamu ya 1994 Il Postino, ambayo ilitokana na riwaya Ardiente Paciencia ya Antonio Skármeta. Umaarufu wa filamu hii duniani ulimpa umaarufu Radford ambaye baadaye alikuja kuwa nyota wa filamu Massimo Troisi. Mkosi ulitokea kutokana na kifo cha Troisi akiwa na miaka 41, siku moja baada ya kukamilika kwa filamu ya Il Postino. Filamu hii ilishinda matuzo mengi duniani, likiwemo tuzo la Filamu bora zaidi ambayo haiku katika lugha ya Kiingereza, BAFTA kwa Radford ambaye alifuzu kwa tuzo la Mwelekezi Bora zaidi kwa ‘’Adapted Screenplay Academy Awards’’.

Mnamo 2000, filamu yake Dancing at the Blue Iguana ilitolewa. Ilitoka nje ya mbinu yake ya kawaida ya kuandika filamu kutokana na vitabu. Radford alishirikiana na David Linter katika utunzi wa filamu hii.

Mnamo 2004 Radford alielekeza filamu The Merchant of Venice (2004). Aliitoa kwa tamthilia ya Shakespeare ya The Merchant of Venice na nyota wa filamu hii ni Al Pacino kama Shylock na Jeremy Irons kama Antonio.

Mnamo 2007 aliwaunganisha tena Demi Moore na Michael Caine (ambao waliwahi kuwa pamoja mnamo 1984 kwa Blame it on Rio) katika filamu yake ya hivi karibuni ya Flawless, ambayo ni hadithi iliyojikitha katika mwaka wa 1960.

Radford pia alielekeza mchezo wake wa kwanza, The Seven Year Itch mnamo 2000, ambao ulitayarishwa na West End Huu ulitokana na filamu ya Billy Wilder iliyoelekezwa mnamo 1955, The Seven Year Itch ambayo inashirikisha Marilyn Monroe kama nyota.

Maisha ya Kibinafsi[hariri | hariri chanzo]

Radford ana mwana wa kiume, Felix wa umri wa miaka 18 kutokana na ndoa yake ya kwanza na Iseult Teran, na mtoto wa kike Amaryllis wa umri wa miaka 4 kutokana na mkewe wa sasa Emma Tweed.

filmografia iliyoteuliwa[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]