Kitenzi kikuu kisaidizi : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika '{{ExamplesSidebar|35%| *Oliver ''''hakutaka''' ''kula'' ugali *Habibu '''angali''' ''anasoma'' darasani *Sisi '''tunataka''' ''kwenda'' '''kuogelea''' mtoni }}...'
(Hakuna tofauti)

Pitio la 13:24, 27 Machi 2014

Mifano
  • Oliver 'hakutaka kula ugali
  • Habibu angali anasoma darasani
  • Sisi tunataka kwenda kuogelea mtoni

Kitenzi kikuu kisaidizi (alama yake ya kiisimu ni: TS) ni kitenzi ambacho hukaa sambamba na kitenzi kikuu ili kukisaidia kitenzi kikuu kukamilisha taarifa. Kitenzi kikuu kisaidizi kikiwa peke yake hakiwezi kutoa taarifa kamili. Hivyo basi kinahitaji msaada/lazima kiambatane na kitenzi kingine (kikuu) ndipo taarifa yake ikamilike.

Mifano
  • Babu yangu alikuwa anaumwa sana (alikuwa ni kitenzi kisaidizi TS - na anaumwa ni kitenzi kikuu T).
  • Wezi walikuwa wanataka kuiba fedha zake (walikuwa na wanataka vyote ni vitenzi visaidizi - isipokuwa kuiba ambapo hapa kimeainishika kama kitenzi kikuu). Kikawaida kitenzi kikuu hukaa mwisho hata kama nyuma yake kutakuwa na wasaidizi kumi.
  • Anna alikuwa anataka kwenda kununua matunda sokoni (alikuwa, anataka, na kwenda vyote ni vitenzi visaidizi isipokuwa kununua inabaki kuwa kitenzi kikuu
  • Upepo ulikuwa umesha ezua mabati yote
  • Juma hakuwa anataka kwenda kununua matunda sokoni

Angalizo: Kitenzi kikuu alama yake ni T kubwa na kitenzi kisaidizi alama yake ni TS.

Tazama pia

Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kitenzi kikuu kisaidizi kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.