Klod

Klod (kwa Kifaransa Cloud; kwa Kilatini Clodoaldus; 522 - 560 hivi) alikuwa padri kutoka ukoo wa kifalme wa Orleans huko Ufaransa [1].
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 7 Septemba[2].
Maisha
[hariri | hariri chanzo]Babu yake alikuwa Klovis I na bibi yake alikuwa mtakatifu Klotilda malkia.
Baba yake, mfalme Klodomer[3], na ndugu zake wawili waliuawa wakiwa bado watoto; yeye tu alinusurika kwa kumkimbilia bibi yake huko Provence[4] na kujinyima haki zote za kurithi. Pia aliwagawia fukara mali iliyombakia.
Baada ya kuishi kama mkaapweke chini ya Severini wa Paris, alipoona anatembelewa na watu wengi kwa ushauri kiasi kwamba hafaidiki na upweke akarudi Paris, alipopokewa kwa furaha.
Watu walimuomba askofu ampe upadrisho (551). Halafu alitoa huduma kwa muda fulani, kisha akarudi upwekeni, na hatimaye akaanzisha abasia karibu na Versailles[5].
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ http://www.santiebeati.it/dettaglio/92412 (Kiitalia)
- ↑ Martyrologium Romanum
- ↑ (Kilatini) Gregorio di Tours, Historiarum Francorum, De interitu Chlodomeris. III, 6
- ↑ (Kilatini) Gregorio di Tours, Historiarum Francorum, De interitu filiorum Chlodemeris. III, 18
- ↑ (Kiingereza) Wafalme wa Kimerovingi
Marejeo ya Kiswahili
[hariri | hariri chanzo]- John Kabeya na wengine - Maisha ya Watakatifu – ed. T.M.P. Book Department – Tabora 1965, 1989, uk. 311
- Pd. Leandry Kimario, O.F.M.Cap. - Mfahamu Mtakatifu Somo Wako - Maisha ya Watakatifu wa Kila Siku pamoja na Watakatifu Wafransisko - Toleo la pili - Dar es Salaam 2021, uk. 266
![]() |
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |