Kisiwa cha Toten

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Kisiwa cha Toten katika hori ya Tanga.
Makaburi kisiwani yalivyokuwa mwaka 1928.

Kisiwa cha Toten ni kisiwa kimojawapo cha Tanzania ambacho kinapatikana katika hori ya Tanga kwenye mwambao wa Bahari ya Hindi.

Kisiwa kina eneo la takriban hektari 16. Kinasemekana kuwa na umbo la tanga la jahazi na hapo ni asili ya jina la mji wa Tanga.

Kuna magofu ya msikiti ya karne ya 17 na makaburi ya karne za 18 na 19. Vipande vya vyungu vimepatikana pia ambavyo vyote ni dalili ya kwamba kisiwa kilikaliwa na watu walioondoka baadaye. [1]

Kabla ya kufika Wazungu kilijulikana kama kisiwa cha Changa. Kumbe jina lililozoeleka sasa linatokana na Kijerumani "Toteninsel" likimaanisha "Kisiwa cha Wafu". Kwasababu Wajerumani walipofika Tanga walisumbuliwa sana na ugonjwa wa malaria, ambao kwa wakati huo haukuwa na tiba, hivyo walitumia kisiwa cha Changa kuwatenga watu wanaougua malaria huku wakifanya utafiti wa tiba ya kufaa ila watu waliofariki wakizikwa kisiwani hapo.

Waingereza walipochukua utawala kutoka kwa Wajerumani walikiita "Toten Island": wakichukua "Toten" kama jina hawakutafsiri maana yake.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Tanga Attractions, Toten Island Island in Tanga, "Lonely Planet Tanzania", tovuti iliangaliwa Februari 2018

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]