Kinga wa Hungaria

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Mt. Kinga.

Kinga wa Hungaria au wa Polandi (pia Kunegunda, Kunigunda, Kioga, Zinga) (Esztergom, Hungaria, 5 Machi 122424 Julai 1292) alikuwa malkia, binti mfalme Bela IV wa Hungaria, na mke wa Boleslao V wa Polandi.[1]

Familia yake asili ilizaa watakatifu mbalimbali, yeye akiwa mmojawapo. Katika ndoa yake inasadikika kwamba waliishi kama kaka na dada.

Pamoja na hayo, Kinga alijitahidi sana kuwatendea kwa huruma mafukara na wagonjwa, wakiwemo wakoma.

Alipofiwa mumewe (1279), aliuza mali yake yote na kugawa mapato yote kwa maskini.

Halafu alikataa madaraka yake ya kiserikali akajiunga na monasteri ya Waklara huko Sandec (Stary Sącz), alipoishi hadi mwisho katika sala tu, asipotaka kabisa itajwe asili yake.

Papa Aleksanda VIII alimtangaza mwenye heri mwaka 1690. Halafu Papa Yohane Paulo II alimtangaza mtakatifu tarehe 16 Juni 1999.

Tangu mwaka 1695 anaheshimiwa kama msimamizi wa Polandi na Lithuania.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Profile, books.google.com; accessed 17 January 2014.
Christian cross.svg Makala hii kuhusu Mkristo huyu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kinga wa Hungaria kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.