Nenda kwa yaliyomo

Ufeministi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Kifeministi)
Maandamano katika Sikukuu ya Kimataifa ya Wanawake huko Dhaka, Bangladesh, tarehe 8 Machi 2005.
Kikosi cha Femen ni Wafeministi wenye itikadi kali.

Ufeministi (kutoka mzizi wa Kilatini femina, yaani wa kike; kwa Kifaransa féminisme linamaanisha harakati ya ukombozi wa wanawake‎) ni jina linalojumlisha aina nyingi za misimamo, itikadi na matapo tofautitofauti yanayochanga lengo kuu la kutetea haki za wanawake dhidi ya ubaguzi wa jinsia uliotawala dunia kwa muda mrefu sana upande wa siasa, uchumi, utamaduni, dini na jamii kwa jumla.[1][2][3]

Wafuasi wa nadharia hii wanashikilia kwamba, pana haja ya kuwa na usawa wa kijinsia licha ya kuwapo kwa tofauti za kimaumbile. [4]

Kati ya haki hizo za msingi, ufeministi umepigania kwa mfano zile za kupiga kura, kupata vyeo serikalini, kufanya kazi, kulipwa mshahara, kumiliki, kupata malezi, kufanya mikataba sawa na wanaume n.k.

Ufeministi umepinga pia ubakaji wa aina zote.[5]

Ufeministi ni kati ya matapo yaliyochangia zaidi mabadiliko katika jamii.[6]

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Katika historia harakati za kudai haki za wanawake zilianza katika Ulaya wakati haki za binadamu zilipoanza kutangazwa, ambazo awali zilijadiliwa kwa wanaume pekee.

Harakati ya kuwapa wanawake haki za kupiga kura kwenye uchaguzi wa kisiasa ilikuwa kampeni ya awali kuanzia karne ya 19, lakini hasa ya 20.

Mikondo tofauti ya ufeministi leo

[hariri | hariri chanzo]
Alama ya ufeministi mkali

Mgawanyiko umeanza kujitokeza kati ya wale wanaotaka wanawake wafanane kabisa na wanaume na wale wanaoona umuhimu wa kutunza upekee wa mwanamke katika uhusiano wa kukamilishana na mwanamume. Kwa mfano:

  • wengine husema wanaume na wanawake wanapaswa kutendewa sawa katika mambo yote. Wanadhani hoja ya jadi kuwa wanawake wana kazi ya kutunza nyumba na kuangalia watoto si sawa: wanawake na wanaume wanapaswa kushiriki katika shughuli zote sawasawa.
  • wengine hukubali kuna tofauti muhimu kati ya jinsia lakini tofauti hizo zisiruhusiwe kuwapa wanaume kipaumbele. Kama wanawake wanapendelea kukaa nyumbani na kuangalia watoto ni sawa, lakini wasilazimishwe kufanya hivyo, nao wanapaswa kupata namna ya malipo kwa kazi hiyo ama sehemu ya mapato ya familia au pia haki za malipo ya pensheni kutoka serikali kwa wakati wa uzee kwa ajili ya miaka waliyoitumia kwa kazi ya nyumbani.
  • wengine husema jamii imepokea utaratibu wake kutokana na mapenzi ya wanaume, hivyo ni lazima kuwa na aina ya mapinduzi katika jamii.
  • kuna wafuasi wa ufeministi wanaoamini ya kwamba hakuna tofauti za maana kati ya jinsia lakini wengine hufundisha kuwa wanawake ni tofauti kabisa na wanaume, na ni muhimu watoe mchango wao wa pekee.

Kuna namna nyingi za kueleza tofauti katika itikadi ya ufeministi lakini hiai hapa ndizo tatu kubwa:

Ufeministi wa kitamaduni - Hii ni aina ya ufeministi ambayo inaangazia ubaguzi katika kawaida ya jamii. Ndio wanoataka utamaduni uthamini hulka za wanawake kuliko ilivyo sasa. Kwa mfano hawa wanaweza kusema wanawake wanachukuliwa vibaya katika vyeo vya juu kutokana na wanaume.

Ufeministi wa uhuru - Hii ni aina ya ufeministi ambayo inaangazia haki za wanawake za kufanya usawa na wanaume hasa. Ndio wanaotaka sheria iruhusu yote yanayoruhusiwa tayari kwa wanaume. Kwa mfano haki za kupiga kura, za kuwania wadhifa wa siasa, au kuvaa mavazi yoyote.

Ufeministi mkali (radical feminism) - Hii ni aina ya ufeministi dubwana kupita nyingine inayodai kwamba hakuna tofauti kati ya wanaume na wanawake ila zile zinazofundishwa na jamii. Kwa mfano, kulingana na itikadi hii, tabia kati ya jinsia siyo ya kibiolojia bali ni ya mafunzo tu. Wafausi hao wanaamini tofauti hizi zipo ili wanaume waweze kudhulumu wanawake.

  1. Hawkesworth, M.E. (2006). Globalization and Feminist Activism. Rowman & Littlefield. ku. 25–27. ISBN 9780742537835.
  2. Beasley, Chris. (1999). What is Feminism?. New York: Sage. ku. 3–11. ISBN 9780761963356.
  3. hooks, bell. (2000). Feminism is for Everybody: Passionate Politics. Pluto Press. ISBN 9780745317335.
  4. K.E. Kipyegon, uk.7
  5. Echols, Alice (1989). Daring to Be Bad: Radical Feminism in America, 1967–1975. Minneapolis: University of Minnesota Press. ISBN 0-8166-1787-2.
  6. Messer-Davidow, Ellen (2002). Disciplining Feminism: From Social Activism to Academic Discourse. Durham, N.C.: Duke University Press. ISBN 0-8223-2843-7.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ufeministi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.