Majadiliano:Ufeministi

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Ee Riccardo umenishinda dakika 5 - hapo chini makala niliyokuwa nikitunga. Sasa nitaangalia baadaye tufanye namna gani. Kipala (majadiliano) 10:41, 16 Mei 2015 (UTC)[jibu]

Maandamano kwenye Siku ya Kimataifa ya Wanawake huko Dhaka, Bangladesh tarehe 8 Machi 2005

Ufeministi (far. féminisme) unamaanisha harakati ya ukombozi wa wanawake‎.

Neno hili linataja jumla ya harakati na itikadi tofautitofauti zinazolenga kufikia usawa wa haki za wanawake katika siasa, uchumi, utamaduni na jamii kote duniani. Wafuasi wa nadharia hii wanashikilia kwamba, pana haja ya kuwa na usawa wa kijinsia licha ya kuwapo kwa tofauti za kimaumbile. [1] Hii ni pamoja kutafuta nafasi sawa kwa wanawake katika elimu na ajira.

Kuna mikondo tofauti za ufeministi

  • wengine husema wanaume na wanawake wanapaswa kutendewa sawa katika mambo yote. Wanadhani ya hoja la kijadi kuwa wanawake wana kazi ya kutunza nyumba na kuangalia watoto si sawa na wanaume sawa na wanawake wanapaswa kushiriki katika shughuli hizi sawa.
  • wengine hukubali kuna tofauti muhimu kati ya jinsia lakinitofauti hizi zisiruhusiwe kuwapa wanauma kipaumbele. Kama wanawake wanapendelea kukaa nyumbani na kuangalia watoto ni sawa lakini wasilazimishwe kufanya hivyo na ya kwamba wanapaswa kupata namna ya malipo kwa kazi hii ama sehemu ya mapato ya familia au pia haki za malipo ya pensheni kutoka serikali kwa wakati wa uzee kwa ajili ya miaka walipotumia kwa kazi ya nyumbani.
  • wengine husema ya kwamba jamii imepokea utaratibu wake kutokana na mapenziy a wanaume hivyo ni lazima kuwa na aina ya mapindizi katika jamii.
  • kuna wafuasi wa ufeministi wanaoamini ya kwamba hakuna tofauti za maana kati ya jinsia lakini wengine hufundisha kuwa wanawake ni tofauti kabisa na wanaume.

Katika historia harakati za kudai haki za wanawake zilianza katika Ulaya wakati haki za binadamu zilianza kutangazwa ambazo awali zilijadiliwa kwa wanaume pekee. Harakati ya kuwapa wanawake haki za kupiga kura kwenye uchaguzi wa kisiasa ilikuwa kempeni ya kwamza kuanzia karne ya 19.


Viungo vya Nje[hariri chanzo]

Keter Ebrahim Kipyegon, Nafasi na utambulisho wa mwanamke katika Natala na Kifo, Nairobi 2013 (inajadili kwa upana ufeministi katika fasihi)

Tovuti ya shirika lisilo la serikali la “Haki za Wanawake na Maendeleo”

Sera ya maendeleo ya wanawake na jinsia, Wizara ya maendeleo ya jamii, wanawake na watoto, Dar es Salaam mwaka 2000

  1. K.E. Kipyegon, uk.7