Jeromu Emiliani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Mt. Jeromu Emiliani.

Jeromu Emiliani (14868 Februari 1537) alikuwa padri na mtawa nchini Italia.

Ametambuliwa na Kanisa Katoliki kuwa mtakatifu na msimamizi wa mayatima.

Sikukuu yake ni tarehe 8 Februari[1].

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Jeromu Emiliani alizaliwa mjini Venisi huko Italia mwaka 1486.

Kwanza alikuwa askari, lakini baadaye akaacha kazi hiyo ili ajitoe mhanga kuwahudumia maskini; akawapa mali yake yote.

Baada ya kupata upadri (1518) alianzisha Utawa wa Makleri ulioitwa Wasomaska, ili kuwasaidia mayatima na maskini.

Alifariki Somasca, karibu na mji wa Bergamo, mwaka 1537.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • "Sala ya Kanisa - Vipindi vya Liturjia", Toleo la Tatu 1996, Ndanda - Peramiho: Benedictine Publications, uk.1283

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Christian cross.svg Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.