James Alexander Stevenson

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

James Alexander Stevenson (1881 - 5 Oktoba 1937) alikuwa mchongaji Mwingereza aliyeumba sanamu mbalimbali pamoja na Sanamu ya Askari iliyoko jijini Dar es Salaam.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Stevenson alizaliwa Chester, Cheshire, Uingereza. Alisoma uchongaji kwenye Royal College of Art na Royal Academy Schools. Alitumia jina la kisanii Myrander, lililounganisha jina la mke wake Myra na jina lake la pili Alexander. Alikuwa mwanachama wa taasisi ya Royal Academy of Arts na Shirika la Kifalme la Wachongaji wa Uingereza.

Kati ya kazi zake zilikuwemo sanamu mbalimbali alizozitengeneza akitumia hasa bronzi. Baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia alichonga sanamu tatu kwa kumbukumbu ya askari wa King`s African Rifles na wapagazi Waafrika waliopiga vita hivyo katika Afrika ya Mashariki, hasa kati ya Uingereza na Ujerumani, ambao wengi wao walikufa. Zilipelekwa Nairobi (Kenyatta Avenue), Mombasa (Jomo Kenyatta Avenue, Mwembe Tayari) na Dar es Salaam (Samora Avenue) [1].

Picha[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Where are the Africans, the missing ˜"feet and hands" of the army of the First World War?, taarifa ya gazeti Standard, Nairobi ya 02.12.2018, iliangaliwa Aprili 2020