James Alexander Stevenson
James Alexander Stevenson (1881 - 5 Oktoba 1937) alikuwa mchongaji Mwingereza aliyeumba sanamu mbalimbali pamoja na Sanamu ya Askari iliyoko jijini Dar es Salaam.
Maisha
[hariri | hariri chanzo]Stevenson alizaliwa Chester, Cheshire, Uingereza. Alisoma uchongaji kwenye Royal College of Art na Royal Academy Schools. Alitumia jina la kisanii Myrander, lililounganisha jina la mke wake Myra na jina lake la pili Alexander. Alikuwa mwanachama wa taasisi ya Royal Academy of Arts na Shirika la Kifalme la Wachongaji wa Uingereza.
Kati ya kazi zake zilikuwemo sanamu mbalimbali alizozitengeneza akitumia hasa bronzi. Baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia alichonga sanamu tatu kwa kumbukumbu ya askari wa King`s African Rifles na wapagazi Waafrika waliopiga vita hivyo katika Afrika ya Mashariki, hasa kati ya Uingereza na Ujerumani, ambao wengi wao walikufa. Zilipelekwa Nairobi (Kenyatta Avenue), Mombasa (Jomo Kenyatta Avenue, Mwembe Tayari) na Dar es Salaam (Samora Avenue) [1].
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Sanamu ya Dar es Salaam
-
Sanamu ya Nairobi
-
Sanamu ya Mombasa inaonyesha mpelelezi (scout), askari Mwarabu, askari wa KAR na mpagazi
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Where are the Africans, the missing ˜"feet and hands" of the army of the First World War?, taarifa ya gazeti Standard, Nairobi ya 02.12.2018, iliangaliwa Aprili 2020
- Kuhusu Stevenson Ilihifadhiwa 3 Juni 2020 kwenye Wayback Machine., tovuti ya Mapping the Practice and Profession of Sculpture in Britain and Ireland 1851-1951
- Kuhusu sanamu ya Mfalme George V iliyochongwa na Stevenson
- Kuhusu ukarabati wa sanamu ya Mombasa na historia ya uchongaji Ilihifadhiwa 20 Aprili 2020 kwenye Wayback Machine.