Ikulu ya Kenya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Ikulu ya Nairobi
Mkurugenzi Mkuu wa WTO Roberto Azevêdo na Rais Uhuru Kenyatta, katika Ikulu (2014)

Ikulu ya Kenya ni makazi rasmi ya Rais wa Kenya. Ilikuwa ni makazi ya Waziri Mkuu wa Kenya kutoka uhuru, tarehe 12 Disemba 1963 hadi Kenya ilipogeuka kuwa jamhuri tarehe 12 Disemba 1964. Imekuwa makazi ya rais tangu siku ya kutangaza jamhuri.[1]

Historia[hariri | hariri chanzo]

Kabla ya ujenzi wa Nyumba ya Serikali (kwa Kiingereza: Government House) jijini Nairobi, makazi ya Gavana wa kwanza yalikuwa katika Nyumba ya Serikali, Mombasa

Nyumba ya Serikali katika Nairobi, Ikulu ya leo, ilijengwa mwaka 1907 katika Nairobi itumike kama makazi rasmi ya Gavana wa Afrika ya Mashariki ya Kiingereza wakati Kenya ilikuwa koloni la Uingereza. Gavana alifanyia kazi rasmi katika ofisi ya zamani ya Kamishna wa Mkoa (ambayo sasa ni turathi ya kitaifa) karibu na Nyayo House na kisha kupumzika katika Nyumba ya Serikali. 

Baada ya uhuru, Nyumba ya Serikali ilipatiwa jina Ikulu[1]

Makazi mengine[hariri | hariri chanzo]

Pamoja na Ikulu ya Nairobi, kuna Ikulu nyingine katika majiji ya Mombasa na Nakuru.

Pia kuna nyumba za makazi katika Eldoret, Sagana, Kisumu na Kakamega. Zimetawanyika kote nchini kumtolea rais makazi aendapo ziara popote nchini.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]