Nyayo House

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Nyayo House ni jumba la ofisi za serikali jijini Nairobi, Kenya. Lilijengwa wakati wa serikali ya rais Daniel Toroitich Arap Moi na kupokea jina lake kutokana na itikadi ya "Nyayo" iliyokuwa wito wa raisi huyu.

Nyayo House ilikamilishwa mwaka 1982 ina ghorofa 27 na urefu wa mita 84.1. Ndani yake kuna ofisi mbalimbali za serikali pamoja na serikali ya mkoa wa Nairobi na idara ya uhamiaji na mengi mengine.

Wakati wa serikali ya Moi ilikuwa pia na sehemu za gereza ambako wafungwa wa kisiasa waliteswa vibaya. Mwaka 2010 wafungwa 21 wa zamani walipewa haki ya dhamana ya milioni KSh 40 kwa mateso waliotendewa katika jela za Nyayo House.[1]

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

  1. FROM NYAYO HOUSE TO GODOWN ARTS CENTER uk. 23