Hamali

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Mahamali wa Japani mnamo 1863/1885 wavusha wateja mtoni
Hamali wa kabila la Sherpa akibeba ubao katika milima ya Himalaya karibu na Mount Everest

Hamali ni mtu anayembebea mtu mwingine mizigo yake.

Mahamali kihistoria[hariri | hariri chanzo]

Katika historia ya kibinadamu watu yaani mahamali walikuwa njia ya kusafirisha mizigo kwa muda mrefu. Katika Asia, Ulaya na Afrika ya Kaskazini wanyama walipatikana walioweza kuchukua kazi hii kama vile farasi, punda, ng'ombe au ngamia. Lakini katika sehemu kubwa ya Afrika na pia Amerika utamaduni asilia ulitegemea nguvu ya mahamali wa kibinadamu. Pia katika maeneo penye milima mikali au misitu minene penye matope wanayama wa kubebea mizigo walishindwa na mizigo ilitegemea nguvu ya kibinadamu.

Katika Afrika kusini ya Sahara biashara ya misafara ilitegemea hasa mahamali.

Mahamali siku hizi[hariri | hariri chanzo]

Siku mahamali wanapatikana kwenye vituo vya usafiri penye watu wengi kama vile kituo cha reli, cha basi au uwanja wa ndege. Kuna pia mahamali wanaosaidia wateja kwenye masoko makubwa. Siku hizi mahamali karibuni wamepotea katika nchi zilizoendelea sana kwa sababu gharama ya maisha imesababisha kupanda kwa mishahara hadi watu wamependelea kubeba mizigo yao wenyewe. Katika nchi kama hizi kokoteni za mzigo ziko tayari kila mahali zinazochukuliwa na wateja au wasafiri kwa hiari yao.

Mahamali kwenye safari za milimani[hariri | hariri chanzo]

Hadi leo kuna mahamali katika maeneo pasipo na barabara hasa mlimani na wasafiri, wapelelezi, wanasayansi au watalii hupaswa kuwakodisha wakitaka kusafiri katika mazingira hiyo.

Watu wanaopanda Mlima Kilimanjaro hupaswa kuwa na mwenji atakayewaongoza lakini kwa kawaida wanaenda pia na hamali anayewabebea mzigo. Sababu kuu ni ya kwamba mtu asiye mwenyeji hukosa nguvu za kubeba mizogo katika kimo kikubwa kwa sababu hajazoea wala kimo wala hewa hivyo humhitaji mwenyeji.

Katika milima ya Himalaya ambayo ni mirefu kushinda Kilimanjaro mahamali ni lazima kabisa. Mara nyingi huitwa kwa jina la "sherpa" ambalo kiasili ni jina la kabila fulani lakini siku hizi neno latumiwa pia kama "hamali".