Habakuki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sanamu ya Habakuki iliyotengenezwa na Donatello, Museo dell'Opera del Duomo, Florence.

Habakuki alikuwa nabii wa Israeli ya Kale aliyeishi na kufanya kazi wakati mmoja na nabii Yeremia (karne ya 7 KK)

Hababuki aliandika kitabu kifupi ambamo alithubutu kumuuliza Mungu kwa nini anaadhibu Israeli vikali kwa mikono ya watu wabaya kuliko wao.

Jibu ni kwamba Mwenyezi Mungu ana njia zake ambazo anaandaa ushindi wa haki: hivyo mwadilifu ataishi kwa imani yake (1:12-2:4).

Usemi huo ukaja kutumika sana katika Agano Jipya. Mtume Paulo ameufanya msingi wa msimamo wake kuwa wokovu unapatikana kwa imani, si kwa kujitahidi kutekeleza masharti yote ya Torati.

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 2 Desemba[1][2].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Habakuki kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.