Gregori wa Nisa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mt. Gregori wa Nisa
(picha ya ukutani wa karne ya 14t, Chora Church, Istanbul, Uturuki.)

Gregori wa Nisa (Neocaesarea, 335Nisa, 395) alikuwa askofu wa Nisa miaka 372 - 376, halafu 378 hadi kifo chake.

Gregori, pamoja na kaka yake Basili Mkuu na rafiki yao Gregori wa Nazianzo wanatajwa kama Mababu wa Kapadokia.

Gregori hakuwa na kipaji cha uongozi cha kaka yake Basili, wala hakuathiri Kanisa kama Gregori wa Nazianzo, lakini alikuwa na akili na elimu kubwa zilizomwezesha kuchangia sana teolojia kuhusu Utatu na maisha ya kiroho. Kwa sababu ya kushika imani sahihi, kaisari Valens, mfuasi wa Ario, alimfukuza jimboni[1].

Anaheshimiwa kama mtakatifu na Kanisa Katoliki, Waorthodoksi, Waorthodoksi wa Mashariki, Walutheri na Waanglikana siku tofautitofauti.

Katika Kanisa la Kilatini ni tarehe 10 Januari[2].

Sala yake[hariri | hariri chanzo]

Ee Mchungaji mwema, unakwenda wapi kuchunga, wewe unayebeba mabegani kundi lako lote?

Kwa kuwa kondoo yule pekee anawakilisha ubinadamu wote uliobeba mabegani mwako.

Unionyeshe mahali pa pumziko, unifikishe kwenye majani mema ya kunilisha, uniite kwa jina, ili mimi pia, niliye kondoo, niweze kusikia sauti yako na kwa hiyo niweze kupata uzima wa milele: “Unionyeshe mpenzi wa roho yangu”.

Ndivyo ninavyokuita, kwa kuwa jina lako liko juu ya kila jina na uelewa, wala ulimwengu wote wa viumbe wenye akili hauwezi kulitaja nakulielewa.

Basi, jina lako, ambamo wema wako unajitokeza, unawakilisha upendo wa roho yangu kwako.

Kwa kuwa ningewezaje kutokupenda, baada ya wewe kunipenda mno? Ulinipenda hivi hata ukatoa uhai wako kwa kundi la malisho yako.

Haiwezekani kufikiria upendo mkuu kuliko huo. Umelipa wokovu wangu kwa uhai wako.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Maandishi yake[hariri | hariri chanzo]

De virginitate

Maandishi yake yote katika lugha asili ya Kigiriki pamoja na ufafanuzi wa Kilatini yanapatikana katika mfululizo Gregorii Nysseni Opera:

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Marejeo mengine[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]