Godfrey Mwampembwa
Godfrey Mwampembwa (anayejulikana kwa jina la kalamu Gado; alizaliwa Dar es Salaam, 6 Agosti 1969) ni mchoraji wa katuni kutoka nchini Tanzania anayeishi Kenya. Katuni zake nyingi zinahusu habari za siasa lakini amechora pia Hekaya za Abunuwasi. [1] Gado ni mchoraji anayechapishwa zaidi katika Afrika ya Mashariki. Kwa zaidi ya miongo miwili alikuwa mchangiaji katika Daily Nation na East African (Kenya), New African (Uingereza), Courrier International (Ufaransa) na Business Day na Sunday Tribune (Afrika Kusini). Alichora pia katuni kwa Le Monde (Ufaransa), Washington Times (Marekani), Der Standard (Austria) na Japan Times (Japani).
Alichangia katika gazeti la Daily Nation karibu kila siku kwa miaka 23 hadi alipofukuzwa kazi kwenye Machi 2016 [2]
Masomo na maisha ya binafsi
[hariri | hariri chanzo]Mwampembwa alianza kuchora alipokuwa bado mtoto wa shule akaanza pia kuchora katuni za kisiasa. Baada ya kumaliza shule alijiunga na Chuo Kikuu cha Ardhi kwa masomo ya usanifu majengo. Alipokuwa mwanafunzi alishiriki katika mashindano ya katuni akasafiri Nairobi kupokea tuzo aliloshinda akapewa nafasi ya ajira palepale[3]. Kwa hiyo baada ya mwaka mmoja aliacha masomo yake na kuwa mchoraji wa katuni wa Nation Media Group huko Kenya. [4] Mnamo mwaka 2000 alisoma uhuishaji wa zamani na filamu katika shule ya filamu huko Vancouver. Mwaka 2015 alitumia kipindi cha mapumziko kwenye Nation Media kwa masomo kwenye Chuo cha Filamu New York (New York Film School).[5]
Amemwoa Stephanie Uwingabe akazaa naye mabinti mawili, Mwaji-Odeta na Keza-Anganile[6].
Kazi
[hariri | hariri chanzo]Gado hutengeneza katuni za kuchekesha yanayohusu habari za siasa ya Afrika ya Mashariki na siasa ya kimataifa.
Alipoanza kuchora katuni nchini Kenya, nchi hiyo ilikuwa kwenye majira ya mabadiliko ya siasa ya vyama vingi. Gado anasemekana alikuwa mchoraji wa kwanza aliyejiamini kumwonyesha rais Arap Moi katika katuni zake. Baada ya huduma ya miaka mingi namna zake ya kuonyesha viongozi wa serikali zilianza kuleta matatizo kwa gazeti la Nation tangu kushtakiwa kwa rais Uhuru Kenyatta pamoja na mwanasiasa na makamu wake William Ruto mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Jinai mnamo mwaka 2010.[7]
Mwaka 2015 alimchora rais Jakaya Kikwete wa Tanzania kama mtu nusu-uchi anayehudumiwa na wanawake warembo waliowakilishi kasoro alizioona katika serikali yake. Gazeti la "The East African" ilibanwa nchini Tanzania kwa mwaka mmoja. Wakati huohuo alimchora makamu wa rais wa Kenya Ruto kwa namna ya kumwunganisha na kashfa ya kutwaa ardhi ya shule mjini Nairobi. Mwampembwa alipumzishwa kazi kwa mwaka mmoja na mwaka 2016 alipokea barua ya kuachishwa kazi.
Tangu kuondoka katika ajira ya Mation Media, Mwampembwa alianza kuchora kwa media ya kimataifa na kuendesha kampuni yake ya Bunimedia. Manmo mwaka 2021 alichangia pia katuni za kila siku kwenye East African Standard.
Tuzo
[hariri | hariri chanzo]Mnamo 1999 Gado alichaguliwa kuwa Mchora Katuni wa Mwaka wa Kenya. [8]
Mnamo 1996 alipewa Tuzo ya Media ya Olimpiki ya Kimataifa kwa media ya kuchapisha [9] na mnamo 1999 alikuwa Mwampembwa Mchora Katuni wa Mwaka Kenya. Alikuwa mmoja wa washiriki kumi na wawili wa maonyesho ya Cartooning for Peace of the United Nations mnamo 2006.
Mnamo 2007 alipewa Tuzo ya Prince Claus kwa mada ya Utamaduni na Mizozo. Majaji walimsifu kwa "katuni zake za ujasiri ambazo zinaonyesha kwa ucheshi mambo ya mizozo ya kijamii na kisiasa, na msukumo wa mapambano ya kujieleza huru."
Mnamo 2014 & 2016, Gado alitajwa na jarida The NewAfrican kama mmoja wa watu 100 wenye ushawishi mkubwa barani Afrika.
Mwaka 2016 Gado alipokea tuzo ya Katuni kwa Amani 2016 aliyekabidhiwa na Kofi Annan kwenye Siku ya Wanahabari Duniani, 2 Mei. [10]
Kazi zake
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Gado". lambiek.net. Iliwekwa mnamo 9 Oktoba 2018.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Kenyan cartoonist fired after mocking president, March 14, 2016 12:01AM The Times
- ↑ [https://www.ft.com/content/67491ade-3ae2-11e7-ac89-b01cc67cfeec Gado, the political cartoonist who satirises Kenya’s president], gazeti la Financial Times tar. 24.05.2017, iliangaliwa Aprili 2020
- ↑ "Report From: Office of International Affairs". www.emory.edu. Iliwekwa mnamo 9 Oktoba 2018.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ [https://businesstoday.co.ke/the-bold-cartoon-that-got-gado-fired-by-nation-media/ The bold cartoon that got GADO fired by Nation Media], tovuti ya businesstoday.co.ke, ya tar. 14.06.2016, iliangaliwa Aprili 2020
- ↑ [http://gadocartoons.com/bio/ Bio], tovuti ya gadocartoons.com, iliangaliwa Aprili 2020
- ↑ [https://www.cnyakundi.com/just-a-reminder-this-is-why-cartoonist-gado-was-fired-from-the-daily-nation/ Just a Reminder : This is why Cartoonist Gado was Fired from the Daily nation], blogu ya Cyprian Nyakundi ya tarehe 13.06.2015, iliangaliwa aprili 2021
- ↑ 8.0 8.1 Pilcher, Tim and Brad Brooks. (Foreword: Dave Gibbons). The Essential Guide to World Comics. Collins and Brown. 2005. 297.
- ↑ Wainaina, Binyavanga (2003). Kwani? 02. Kwani Archive Online. uk. 158. ISBN 9789966983626.
- ↑ Radoli, Lydia. "Celebrated Kenyan Cartoonist, GADO Wins the International Editorial Cartoons Prize". Mkenya Ujerumani. Iliwekwa mnamo 2017-03-02.
- ↑ Repetti, Massimo (1 Juni 2007). "African Wave: Specificity and Cosmopolitanism in African Comics". African Arts. 40 (2): 16–35. doi:10.1162/afar.2007.40.2.16. Iliwekwa mnamo 9 Oktoba 2018.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- [http://web.archive.org/20210624093129/http://www.gadocartoons.com/ Ilihifadhiwa 24 Juni 2021 kwenye Wayback Machine. Tovuti rasmi ya Gado]
- Wavuti ya zamani ya Gado (kumbukumbu)
- [http://web.archive.org/20140813200755/http://www.wasaniikenya.com/arts-design/godfrey-mwampembwa-gado.html Ilihifadhiwa 13 Agosti 2014 kwenye Wayback Machine.]