Nenda kwa yaliyomo

Gari safi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Gari Safi)
Toyota Prius
Toyota Prius

Gari safi (kwa Kiingereza green vehicle au clean vehicle) ni gari lililotengenezwa kwa teknolojia ya kisasa kwa lengo la kupunguza athira mbaya kwa mazingira. Magari ya aina hii hayatoi moshi na hayatumii petroli au diseli katika kupata kawi. Kwa sababu hiyo, huwa halina maafa kwa mazingira. Nchi kama zile za Ulaya na jimbo la California vimeweka mikakati kwa kutambua gari safi lisitumie fueli ambayo itaathiri mazingira vibaya.

Gari hili huenda likatumia kawi kama ya betri, hidrojeni au ethanoli.

Mikakati ya utumizi mzuri wa kawi

[hariri | hariri chanzo]

Gari hili hutumia mikakati ifuatayo kuhakikisha kuwa halitaharibu mazingira au kutumia kawi nyingi.

  1. Njia badala ya propulsion kama vile utumizi wa biofuel badala ya petroli
  2. Utoaji wa vitu vinavyofanya gari liwe zito na kwa njia hii kupunguza kawi inayohitajika kuliendesha
  3. Kufanya ukarabati wakati unaofaa kama vile ukarabati wa injini na magurudumu.

Ubora wa kutumia gari safi

[hariri | hariri chanzo]

Mazingira

[hariri | hariri chanzo]

Utumizi wa gari kijani kibichi husaidia katika kuhifadhi mazingira na hali ya hewa. Wataalamu wa masuala ya hali ya hewa wameonyesha kuwa kuachiliwa kwa uchafu unaotokana na petrolo pamoja na diseli kunachangia katika uharibifu wa ozone layer na hili linafanya ardhi iwe na joto kupindukia pamoja na hewa isiyoweza kukadirika.

Kuachiliwa kwa uchafu wa petroli na diseli kumechangia pakubwa katika kudhoofika kwa hali ya afya ya watu na kukawa na magonjwa ya mapafu na saratani ya mfumo wa kupumua.

Utumizi wa magari kijani kibichi umesaidia katika uchumi kwani hayatumii pesa nyingi kama mengine ya petroli.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.