Uchafu
Mandhari
Uchafu ni yale yanayosababisha kitu au mtu kukosa usafi. Kwa kawaida ni vitu kama vile vumbi, matope, kinyesi au mabaki ya chakula. Kwa Kiswahili "uchafu" unaweza kumaanisha pia hali ya kukosa usafi wa kimaadili au wa kiroho.
Kama mata fulani inatazamwa kuwa "chafu" hutegemea wakati, mahali na utamaduni wa mtazamaji. Kwa mtazamo huo uchafu ni mata inayopatikana mahali pasipotakiwa na wakati usiotakiwa. Kwa mfano:
- ardhi kwenye shamba ni malighafi muhimu yenye thamani, lakini kwenye nguo ardhi hiyohiyo ni uchafu
- mavumbi katika mazingira makavu ni jambo la kawaida, yaani punje ndogo za mata thabiti zinazoweza kusukumwa na upepo na kuelea hewani kwa muda hadi kutelemka tena. Kama mavumbi yanatelemka na kukaa kwenye nguo, nywele za watu, dirishani au kwenye gari huitwa uchafu
- rangi hununuliwa hata kwa bei kubwa ili kuipaka kwenye vyombo, nyumba au samani. Rangi ileile ikitiririka kwenye ngozi au kwenye nguo huwa uchafu
Kujisomea
[hariri | hariri chanzo]- Terence McLaughlin (1971), Dirt: a social history as seen through the uses and abuses of dirt, Stein and Day, ISBN 9780812814125
- Suellen Hoy (1996), Chasing Dirt: The American Pursuit of Cleanliness, Oxford University Press, ISBN 9780195111286
- Pamela Janet Wood (2005), Dirt: filth and decay in a new world arcadia, Auckland University Press, ISBN 9781869403485
- Ben Campkin, Rosie Cox (2007), Dirt: new geographies of cleanliness and contamination, I.B. Tauris, ISBN 9781845116729
- Virginia Smith; na wenz. (2011), Dirt: The Filthy Reality of Everyday Life, Profile Books Limited, ISBN 9781846684791
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Uchafu kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |