Nenda kwa yaliyomo

Forest (Mbeya mjini)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Kata ya Forest
Kata ya Forest is located in Tanzania
Kata ya Forest
Kata ya Forest

Mahali pa Foresti katika Tanzania

Majiranukta: 8°53′24″S 33°25′48″E / 8.89000°S 33.43000°E / -8.89000; 33.43000
Nchi Tanzania
Mkoa Mbeya
Wilaya Mbeya Mjini
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 9,774

Forest ni kata ya Mbeya Mjini katika Mkoa wa Mbeya, Tanzania yenye Postikodi namba 53103.

Forest iko ng'ambo ya barabara kuu ya TANZAM kati ya Mwanjelva na Mabatini. Imeanzishwa tangu miaka ya 1980 katika eneo lenye msitu wa milingoti ulioanza kando ya barabara kuu ukitazama Mabatini. Shabaha ya kuanzisha eneo hili ni kuwa na kitovu kipya cha manispaa ya Mbeya kwa sababu mji wa kale hauna nafasi tena kwa upanuzi wa huduma za serikali na biashara.

Kati ya majengo ya kwanza ya Foresti, mojawapo lilikuwa hospitali ya mkoa.

Katika sensa iliyofanyika mwaka 2022 wakazi walihesabika kuwa 9,774 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 6,649 [2] walioishi humo.

  1. https://www.nbs.go.tz
  2. "Sensa ya 2012, Mbeya - Mbeya MC" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2004-01-02. Iliwekwa mnamo 2017-03-14.
Kata za Jiji la Mbeya - Tanzania

ForestGhanaIdudaIganjoIganzoIgawiloIlemiIlombaIsangaIsyesyeItaganoItendeIteziItijiIwambiIyelaIyungaIziwaKalobeMaangaMabatiniMaendeleoMajengoMbalizi RoadMwakibeteMwasangaMwasenkwaNondeNsalagaNsohoNzovweRuandaSindeSisimbaTembelaUyole


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Mbeya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Forest (Mbeya mjini) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.