Fiziolojia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Fiziolojia ni utafiti wa jinsi viumbe vinavyofanya kazi. Wanaikolojia wanaweza kujifunza jinsi viungo vya mwili vinavyofanya kazi pamoja ili kufanya mambo kutokea.

Somo hili mara nyingi hugawanyika katika kategoria tatu:

Kwa binadamu, kwa mfano, homoni za mmeng'enyo wa chakula na kemikali nyingine hufanywa na tumbo, ini na kongosho. Kusinyaa kwa misuli hutokea kwa sababu ya ujumbe wa kikemikali uliofanywa na neva za hiyo misuli.

Kwa kujifunza jinsi mwili hufanya kazi kwa kawaida, wanafiziolojia na madaktari wanaweza kuelewa vizuri kinachotokea wakati viungo havifanyi kazi kawaida.

Kwa mfano, ufahamu wa jinsi kazi ya tezi ya thairoidi imesaidia katika kutibu rovu. Uchunguzi wa mfumo wa mzunguko wa damu na wa mfumo wa neva umewasaidia madaktari kuelewa na kutibu magonjwa kama vile magonjwa ya moyo, kiharusi na shinikizo la damu.

Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Fiziolojia kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.