Kiharusi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Kiharusi (kwa Kiingereza stroke) ni ugonjwa unaoleta hali ya mwili kupooza kutokana na matatizo kwenye mishipa ya damu inayolisha ubongo.

Katika tiba kiharusi ni upotevu wa uwezo wa ubongo unaoendelea haraka. Sababu yake ni tatizo katika mishipa inayopeleka damu kwenda ubongo.

Matatizo hayo ni ama kuzibwa ama kupasuka kwa mishipa ya damu. Seli za ubongo hufa haraka zisipopata oksijeni na lishe ya kawaida ambayo yote haya hufika kwa njia ya damu.

Kiharusi ni hali ya dharura inayoweza kutibiwa kama tatizo linatambuliwa na kutibiwa haraka. Lisipotibiwa husababisha viwango mbalimbali vya kipooza mwilini.

Shinikizo la juu la damu, kisukari, chakula chenye mafuta mengi au kuvuta sigara huongeza hatari ya kupatwa na kiharusi.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Morpho didius Male Dos MHNT.jpg Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kiharusi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.