Rovu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Rovu (pia goita, kutoka Kiingereza: goitre) ni uvimbe wa shingo unaosababishwa na kukuzwa kwa tezishingo, tezi iliyopo upande wa mbele wa shingo.

Ugonjwa huo kwa kawaida unatokana na ukosefu wa iodini kwenye mwili[1] na unajitokeza kwa kuvimba shingo[2][3].

Muonekano[hariri | hariri chanzo]

Tezishingo inaweza kuongezeka kwa sababu mbalimbali na kuonekana kama uvimbe mdogo hadi mkubwa. Asilimia 90 za rovu zinasababishwa na uhaba wa madini ya iodini kwenye ardhi ya eneo fulani; penye iodini ya kutosha, madini hiyo hupatikana pia kwenye maji na matunda hivyo watu wanaipata kupitia chakula.

Picha[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. R. Hörmann: Schilddrüsenkrankheiten. ABW-Wissenschaftsverlag, 4. Auflage 2005, Seite 15–37. ISBN|3-936072-27-2
  2. Thyroid Nodules and Swellings - British Thyroid Foundation (en-gb). Jalada kutoka ya awali juu ya 2019-10-23. Iliwekwa mnamo 2020-09-11.
  3. Goitre - NHS Choices (en) (2017-10-19).
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Rovu kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.