Filipo Smaldone
Mandhari
Filipo Smaldone (Napoli, Campania, Italia, 27 Julai 1848 – Lecce, Puglia, 4 Juni 1923) alikuwa padri wa Kanisa Katoliki aliyeshughulikia maisha yake yote malezi ya kiutu na ya Kikristo ya mayatima, mabubu na viziwi akaanzisha shirika la kitawa la Masista Wasalesiani wa Mioyo Mitakatifu.
Alikuwa pia na uwezo mkubwa wa kuhubiri na kutoa katekesi.
Papa Yohane Paulo II alimtangaza mwenye heri tarehe 12 Mei 1996 halafu Papa Benedikto XVI alimtangaza mtakatifu tarehe 15 Oktoba 2006.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake.[1]
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Hagiography Circle
- Saints SQPN
- Catholic Forum
- Salesian Missions Ilihifadhiwa 24 Julai 2008 kwenye Wayback Machine.
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |