Visiwa vya Falkland
| |||||
Kaulimbiu ya taifa: "Desire the right" | |||||
Wimbo wa taifa: "God Save the Queen" | |||||
Mji mkuu | Stanley | ||||
Mji mkubwa nchini | Stanley | ||||
Lugha rasmi | Kiingereza | ||||
Serikali | Eneo la ng'ambo la Uingereza Elizabeth II wa Uingereza | ||||
Eneo la ng'ambo la Uingereza Siku ya uhuru (Ushindi juu ya Argentina) |
14 Juni 1982 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
12,173 km² (162) 0 | ||||
Idadi ya watu - Julai 2008 kadirio - Msongamano wa watu |
3,140 [1] (217) 0.26/km² (240) | ||||
Fedha | Falkland Islands pound (FKP )
| ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
(UTC-4) (UTC-3) | ||||
Intaneti TLD | .fk | ||||
Kodi ya simu | +500
|
Visiwa vya Falkland (kwa Kiingereza: Falkland Islands; kwa Kihispania Islas Malvinas) ni funguvisiwa katika bahari ya Atlantiki ya kusini takriban km 450 mbele ya pwani ya Argentina.
Falkland ni eneo la ng'ambo la Uingereza linalodaiwa na Argentina kama sehemu yake. Hivyo mwaka 1982 jeshi la Argentina ilivamia visiwa vikuu. Uingereza ilijibu kivita ikapeleka wanajeshi huko na baada ya vita vifupi vya wiki 6 Argentina ilishindwa; takriban wanajeshi 1,000 waliuawa.
Jiografia
[hariri | hariri chanzo]Funguvisiwa lina takriban visiwa 200. Viwili ambavyo ni vikubwa ni Falkland Magharibi na Falkland Mashariki na kila kimoja huwa na eneo la takriban km² 6,000. Mwinuko mkubwa ni mlima Usborne (Kihispania: Cerro Alberdi) wenye kimo cha mita 708 juu ya uwiano wa bahari.
Hali ya hewa ni baridi na kuna mvua nyingi. Halijoto ya wastani ni 5 °C pekee. Kwa sababu hiyo mimea ni hasa nyasi; kutokana na baridi miti haizidi kimo cha mita 1.
Watu
[hariri | hariri chanzo]Idadi ya wakazi imepita 3,000 na wote hao ni Waingereza wanaosema Kiingereza. Wanajipatia riziki zao kwa uvuvi na ufugaji wa kondoo.
Upande wa dini, 66% ni Wakristo, hasa Waanglikana, lakini pia Wakatoliki na wengineo. 32% hawana dini yoyote.
Mji pekee ambao ni pia makao makuu ya utawala ni Port Stanley kwenye kisiwa cha mashariki wenye wakazi 2,100. Pamoja na wakazi kuna wanajeshi Waingereza 1,500.
Barabara ya lami ya pekee kisiwani ni ile inayounganisha Stanley na kituo cha kijeshi kwa umbali wa kilomita 50.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Falkland Islands (Islas Malvinas)". CIA. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-07-02. Iliwekwa mnamo 2010-03-05.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- L.L. Ivanov et al.. The Future of the Falkland Islands and Its People. Sofia: Manfred Wörner Foundation, 2003. 96 pp. ISBN 954-91503-1-3 (Capítulo principal en español)
- Carlos Escudé y Andrés Cisneros, dir. Historia general de las relaciones exteriores de la República Argentina. Archived 2007-05-28 at Archive.today Obra desarrollada y publicada bajo los auspicios del Consejo Argentino para las Relaciones Internacionales (CARI). Buenos Aires: GEL/Nuevohacer, 2000. ISBN 950-694-546-2 (en castellano)
- Graham Pascoe and Peter Pepper. Getting it right: The real history of the Falklands/Malvinas. Ilihifadhiwa 26 Julai 2011 kwenye Wayback Machine. Mei 2008.
- D.W. Greig, Sovereignty and the Falkland Islands Crisis. Austrialian Year Book of International Law. Vol. 8 (1983). pp. 20-70. ISSN: 0084-7658
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- http://www.pcgn.org.uk/Falkland%20Islands-July2006.pdf Archived 2014-04-02 at the UK Government Web Archive
Makala hii kuhusu maeneo ya Amerika Kusini bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Visiwa vya Falkland kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |