Eukeri wa Lyon
Eukeri wa Lyon (380 hivi - 449 hivi) alikuwa seneta wa Dola la Roma, halafu askofu mkuu wa mji huo wa Gallia (leo Ufaransa)[1][2].
Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 16 Novemba[3].
Maisha na maandishi
[hariri | hariri chanzo]Kisha kufiwa mke wake Galla, alitawa pamoja na wanae Verano na Saloni katika monasteri ya Lérins, iliyoanzishwa na Honorati wa Arles juu ya kisiwa karibu na Antibes.
Baadaye alihamia kisiwa cha Lerona (sasa Sainte-Marguerite), akisoma na kujitesa kwa lengo la kujiunga na Mababu wa jangwani.
Kumbe Yohane Kasiano alifika huko Marseille na kuandika sehemu ya pili ya Collationes (namba 11-17) kwa heshima ya Eukeri na Honoratus.
Wakati huohuo Eukeri aliandika De laude Eremi ("Sifa ya Jangwa") kwa askofu Hilari wa Arles.[4]
Pia aliandika Epistola paraenetica ad Valerianum cognatum, de contemptu mundi kuhusu kudharau ulimwengu.
Liber formularum spiritalis intelligentiae inatetea uhalali wa kufafanua kiroho Biblia.
Kati ya maandishi yake kuna pia Institutiones ad Salonium, barua na homilia kadhaa, wasifu wa wafiadini wengi n.k.
Kutokana na sifa yake, alichaguliwa kuwa askofu wa Lyon mwaka 434 hivi; kwa msingi huo hakika alihudhuria Mtaguso wa Orange (441) akaendelea na cheo hicho hadi kifo chake.[4]
Hapo mwanae Verano alishika nafasi yake, na mwanae mwingine, Saloni, akawa askofu wa Geneva.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
- Mababu wa Kanisa
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Dictionary of Christian Biography and Literature to the End of the Sixth Century A.D., with an Account of the Principal Sects and Heresies. | Christian Classics Ethereal Library
- ↑ https://www.santiebeati.it/dettaglio/77840
- ↑ Martyrologium Romanum
- ↑ 4.0 4.1 Clugnet, Léon. "St. Eucherius." The Catholic Encyclopedia Vol. 5. New York: Robert Appleton Company, 1909. 20 October 2017
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Salvator Pricoco, 1965. Eucherii De Laude eremi (University of Catania) This edition establishes the best, most recent Latin text.
- Bishop of Tours Gregory, Historia Francorum (The History of the Franks) (London, England: Penguin Books, Ltd., 1974).
- Ford Mommaerts-Browne, "A Speculation", http://archiver.rootsweb.ancestry.com/th/read/GEN-ANCIENT/2004-03/1079586413 Archived 13 Februari 2015 at the Wayback Machine..
- Sidonius Apollinaris, The Letters of Sidonius (Oxford: Clarendon, 1915) (orig.), pp. clx-clxxxiii; List of Correspondents, Notes, V.ix.1.
- K. Pollmann, "Poetry and Suffering: Metrical Paraphrases of Eucherius of Lyons’ Passio Acaunensium Martyrum," in Willemien Otten and Karla Pollmann (eds), Poetry and Exegesis in Premodern Latin Christianity: The Encounter between Classical and Christian Strategies of Interpretation (Leiden and Boston: Brill, 2007) (Supplements to Vigiliae Christianae, 87).
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Henry Wace, A Dictionary of Christian Biography and Literature: Eucherius
- Edgar Henneke in The New Schaff-Herzog Encyclopedia of Religious Knowledge: Archived 2013-04-14 at Archive.today Eucherius
- The World Contemned (De Contemptu mundi) (in English, translated by Henry Vaughan, 1654)
- De laude eremi Archived 7 Septemba 2005 at the Wayback Machine. (in Latin) at The Latin Library
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |