Verano wa Vence

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Verano wa Vence (alifariki 480 hivi) alikuwa askofu wa 4 wa mji huo wa Gaul (leo Ufaransa).

Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 11 Novemba[1].

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Kisha kufiwa mama yake Galla, alitawa pamoja na baba yake, Eukeri wa Lyon, na ndugu yake Salonius katika monasteri ya Lérins, iliyoanzishwa na Honoratus juu ya kisiwa karibu na Antibes[2].

Kutokana na sifa yake, baba yake alichaguliwa kuwa askofu wa Lyon mwaka 434 hivi akaendelea na cheo hicho hadi kifo chake.

Hapo Verano alishika nafasi yake[3] , na mwanae mwingine, Salonius, akawa askofu wa Geneva.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Gregori wa Tours, Historia Francorum (The History of the Franks) (London, England: Penguin Books, Ltd., 1974).
Christian cross.svg Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.