Nenda kwa yaliyomo

Mwogeleaji-juuchini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Enithares)
Mwogeleaji-juuchini
Enithares sp.
Enithares sp.
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye mwili wa pingili na miguu ya kuunga wasio na ugwe wa mgongo kama wadudu, nge, buibui)
Nusufaila: Hexapoda (Arithropodi wenye miguu sita)
(bila tabaka): Dicondylia (Wadudu walio na mandibula zenye condyle mbili)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Nusungeli: Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Oda ya juu: Paraneoptera
Oda: Hemiptera
Nusuoda: Heteroptera
Oda ya chini: Nepomorpha
Familia ya juu: Notonectoidea
Familia: Notonectidae
Leach, 1815
Ngazi za chini

Nusufamilia 2, jenasi 11:

Waogeleaji-juuchini ni wadudu wadogo wa maji wa familia Notonectidae katika oda ya chini Nepomorpha ya oda Hemiptera wanaoogelea mgongo ukiwa chini. Familia hii ina takriban spishi 400 duniani kote na angalau 20 katika Afrika ya Mashariki. Wadudu hawa ni mbuai.

Waogeleaji-juuchini wana urefu wa mm 5-16. Mwili wao umerefuka na kuwa mwembamba na kama duaradufu wenye miguu mirefu ya nyuma kama makasia. Sehemu za kinywa chao zina umbo la pia na hutumiwa kutoboa mbuawa wao. Wanafanana na kunguni-makasia, lakini wale wa mwisho hawaogelei juu chini. Pia hukosa mistari myeusi sambamba kwenye mgongo wa mwili ambayo kunguni-makasia wanayo[1].

Biolojia

[hariri | hariri chanzo]

Wadudu hawa huogelea chini ya uso wa maji na kuwinda mawindo madogo hadi mara mbili ya ukubwa wao, kama vile wadudu, ndubwi na samaki wadogo. Wanatoboa mbuawa wao kwa sehemu zao kali za kinywa na kuingiza mate ambayo hutiisha mbuawa na kumfanya ndani yake kuwa kiowevu. Kiowevu hiki kisha hufyonzwa. Wadudu wanaoanguka ndani ya maji pia vinashambuliwa, ambayo inafanywa rahisi kwa kuogelea juu chini. Watu wanaweza kuumwa, jambo linalowapa jina lao mbadala la nyigu-maji. Walakini, hii ni nadra isipokuwa washikwe kwa mkono.

Waogeleaji-juuchini huishi katika maji matamu ambayo yana vitu vingi vya kioganiki, kama maziwa, mabwawa, mito inayotiririka polepole, vinamasi na hata bafu za ndege. Wana mabawa yaliyostawi vizuri na yanayowawezesha kufika makazi mapya. Mwili wao, hasa mabawa ya mbele, umefunikwa kwa nywele ndogo sana zinazoelekea ndani ambazo waogeleaji-juuchini hutumia kunasa mapovu ya hewa, ambayo inaongeza muda wanaoweza kutumia chini ya maji. Mdudu anapomaliza chanzo chake cha oksijeni, lazima arudi kwenye uso ili kupata hewa zaidi[2]. Spishi fulani, k.m. katika jenasi Anisops na Buenoa, huzalisha hemoglobini katika seli kubwa za trakea za fumbatio, ambayo huwaruhusu kubaki chini ya maji kwa muda mrefu zaidi.[3].

Spishi kadhaa za Afrika ya Mashariki

[hariri | hariri chanzo]
  • Anisops amaryllis
  • Anisops balcis
  • Anisops debilis
  • Anisops elegans
  • Anisops eros
  • Anisops hancocki
  • Anisops jaczewskii
  • Anisops leesoniana
  • Anisops magnadens
  • Anisops pellucens
  • Anisops psyche
  • Anisops sardea
  • Anisops varia
  • Anisops wakefieldi
  • Anisops worthingtoni
  • Enithares sobria
  • Enithares v-flavum

Kutazama

[hariri | hariri chanzo]

Waogeleaji-juuchini katika bwawa

  1. https://pondinformer.com/backswimmers-notonectidae/
  2. https://www.beilstein-journals.org/bjnano/articles/9/282/
  3. Wawrowski (2012) Characterization of the hemoglobin of the backswimmer Anisops deanei (Hemiptera) Insect Biochemistry and Molecular Biology 42: 603-609.