Nenda kwa yaliyomo

Dominiko Loricatus

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mt. Dominiko Loricatus kadiri ya M. de Vos.

Dominiko Loricatus, O.S.B. Cam. (kwa Kiitalia: San Domenico Loricato; 995 - 1060), alikuwa mmonaki wa Italia mzaliwa wa kijiji cha Luceolis karibu na Cantiano (leo katika mkoa wa Marche).

Baba yake, akitamani maendeleo, alitoa rushwa ili huyo mwanae mdogo apewe upadrisho. Dominiko alipopata habari aliamua kushika maisha magumu na kufanya toba kali kama mkaapweke, akajiunga na monasteri ya Wakamaldoli huko Fonte Avellana, akiwa na Petro Damiani kama mlezi.

Baadaye huyo alimtuma kuongoza jumuia mpya ya wakaapweke kwenye mlima San Vicino akaandika habari za maisha yake ya ajabu.

Jina "Loricatus" lilitokana na mkanda wa chuma aliouvaa mfululizo kubana kiuno chake[1].

Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 14 Oktoba[2].

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.