Dionysius Mwareopago

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha takatifu ya Mt. Dionysius kutoka Ugiriki.
Opera omnia, 1756.

Dionysius Mwareopago (kwa Kigiriki Διονύσιος ὁ Ἀρεοπαγίτης; alifariki 95 hivi) alikuwa askofu wa kwanza wa Athene, Ugiriki[1].

Umaarufu wake umetokana na Mdo 17:34 kusimulia kwamba alikuwa kati ya wachache waliosadiki hotuba aliyoitoa Mtume Paulo katika Areopago kuhusu Kristo na ufufuko.

Umaarufu uliongezeka baada ya mwanafalsafa asiyejulikana kutoka Siria kuandika vitabu mbalimbali akitumia jina la Dyonisius huyo mwanzoni mwa karne ya 6.

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu mfiadini[2].

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 3 Oktoba[3].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Eusebius, Historia Ecclesiae III: iv
  2. Vetus Martyrologium Romanum: "Athenis, Dionysii Areopagitae, sub Adriano diversis tormentis passi, ut Aristides testis est in opere quod de Christiana religione composuit"
  3. Martyrologium Romanum

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Owen Gingerich, The Book Nobody Read, Penguin Books, 2004, pp. 190–191

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Dionysius Mwareopago kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.