Desmodium uncinatum

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Desmodium uncinatum
Majani na maua
Majani na maua
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Planta (mimea)
(bila tabaka): Angiospermae (Mimea inayotoa maua)
(bila tabaka): Eudicots (Mimea ambayo mche wao una majani mawili)
(bila tabaka): Rosids (Mimea kama mwaridi)
Oda: Fabales (Mimea kama mharagwe)
Familia: Fabaceae (Mimea iliyo na mnasaba na mharagwe)
Jenasi: Desmodium
Desv.
Spishi: D. uncinatum
(Jacq. DC.

Desmodium uncinatum (kwa Kiing. silverleaf desmodium) ni spishi ya mmea inayotoa maua katika familia ya Fabaceae yenye asili ya Amerika ya Kusini. Mmea huu umeletwa katika maeneo mbalimbali ya Afrika, Uhindi, Nyugini, Australia na Hawaii kama malisho ya mifugo[1].

Japo hupandwa zaidi kama malisho ila pia unaweza kulisha mifungo kwa kuikata na kulisha chaani au kusindika kama malisho kavu. Vile vile hutumika kama mimea ya kufunika ardhi kwenye mashamba au kama matandazo[2]. Huko Australia na Hawaii unachukuliwa kuwa mmea vamizi[2].

Spishi hii ya Desmodium pia inatumika katika teknolojia ya sukuma-vuta ya kudhibiti wa wadudu waharibifu wa mazao ya nafaka. D. uncinatum hupandwa katikati ya mistari ya mazao ya nafaka kama muhindi au mtama ili kudhibiti funza wa mabua (stemborers) pamoja na viwavijeshi, haswa nchini Ethiopia, Kenya, Tanzania na Uganda. Japokua kuna spishi nyingi za Desmodium, D. uncinatum pamoja na D. intortum (greenleaf desmodium) ndio spishi za Desmodium ambazo hutumika zaidi kwenye kilimo mseto cha sukuma-vuta. [3] [4]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Desmodium uncinatum (Jacq.) DC.. Plants of the World Online. Board of Trustees of the Royal Botanic Gardens, Kew. Iliwekwa mnamo 23 June 2021.
  2. 2.0 2.1 Heuzé (7 October 2015). Silverleaf desmodium (Desmodium uncinatum). Feedipedia – Animal Feed Resources Information System. Feedipedia, a programme by INRAE, CIRAD, AFZ and FAO. Iliwekwa mnamo 23 June 2021.
  3. Pickett, John A; Woodcock, Christine M; Midega, Charles AO; Khan, Zeyaur R (2014). "Push–pull farming systems". Current Opinion in Biotechnology 26: 125–132. doi:10.1016/j.copbio.2013.12.006. Retrieved 22 March 2022. 
  4. Khan, Zeyaur R; Midega, Charles AO; Bruce, Toby J. A.; Hooper, Anthony M; Pickett, John A (2010). "Exploiting phytochemicals for developing a ‘push–pull’ crop protection strategy for cereal farmers in Africa". Journal of Experimental Botany 61 (15): 4185–4196. doi:10.1093/jxb/erq229. Retrieved 22 March 2022.