Nenda kwa yaliyomo

Fabaceae

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Fabaceae
Ua la Centrosema pubescens, mmea kwenye familia ya Fabaceae
Ua la Centrosema pubescens, mmea kwenye familia ya Fabaceae
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Planta (mimea)
(bila tabaka): Angiospermae (Mimea inayotoa maua)
(bila tabaka): Eudicots (Mimea ambayo mche wao una majani mawili)
(bila tabaka): Rosids (Mimea kama mwaridi)
Oda: Fabales (Mimea kama mharagwe)
Familia: Fabaceae (Mimea iliyo na mnasaba na mharagwe)
Lindl.
Ngazi za chini

Nusufamilia 6:

Fabaceae au Leguminosae, inayojulikana kama familia ya mimea ya jamii ya mkunde na mimea aina ya mharagwe, ni familia kubwa ya mimea yenye maua iliyo na umuhimu kiuchumi na kibiolojia. Familia hii inajumuisha miti, vichaka na mimea ya muda na ya msimu, na inatambuliwa kwa urahisi kwa kupitia matunda (kunde) na majani yake. Mimea mingi ya jamii ya mkunde ina maua na matunda ya kipekee.

Familia hii imesambaa maeneo mengi duniani na ni familia ya tatu kwa ukubwa kwa mimea ya nchi kavu kwa kuzingatia idadi ya spishi, ikipitwa na familia ya Okidi na Asteraceae pekee. Inajumuisha takribani jenasi 751 zenye spishi zipatazo 19,000. [1] [2]

Jenasi tano kubwa zaidi za familia hii ni Astragalus (zaidi ya spishi 3,000), Acacia (spishi zaidi ya 900), Indigofera (karibu spishi 700), Crotalaria (spishi karibu 700), na Mimosa (karibu spishi 400). Jenasi hizi kwa pamoja zinabeba walau robo ya spishi zote za mimea ya jamii ya mkunde. Spishi 19,000 za jamii ya mkunde zinazojulikana hadi sasa kwa pamoja zinatengeneza karibu 7% ya spishi zote za mimea yenye maua. [3] Mimea ya familia hii ndiyo inayopatikana kwa wingi zaidi katika misitu ya mvua ya kitropiki na misitu kavu ya Amerika na Afrika. [4]

Tafiti za hivi karibuni zilizotumia njia za kimolekula na maumbile zinaonyesha kwamba familia ya Fabaceae ni kundi la kijenetiki kutoka kwa mhenga mmoja. [5] Swala hili linapata mkazo kutokana na uhusiano kati ya makundi ya mimea ndani ya familia hii, uhusiano wa familia hii mimea inayokaribiana nayo pamoja na tafiti za jenetika zinazotumia Asidi Kiinideoksiribo.[6][7][8]. Tafiti hizi zimeonyesha kwamba mimea ya familia ya Fabaceae ni kundi lenye jadi moja linalohusiana kwa ukaribu na familia za Polygalaceae, Surianaceae na Quillajaceae ambazo kwa pamoja zipo chini ya oda ya Fabales.[9]

Baadhi ya mimea ya familia ya Leguminosae imekua chanzo kikuu cha chakula cha binadamu kwa milenia nyingi pamoja na nafaka, baadhi ya matunda na vyakula vya mizizi vya kitropiki. Matumizi ya vyakula hivi yanahusiana kwa ukaribu na mageuko ya binadamu.[10] Familia hii inajumuisha mimea mingi yenye umuhimu kwanye kilimo na chakula, ikiwemo Glycine max (maharagwe ya soya), Phaseolus (maharagwe), Pisum sativum (njegere), Cicer arietinum (njegere kubwa), Medicago sativa (luseni), Arachis hypogaea (karanga), Ceratonia siliqua (karuba), na Glycyrrhiza glabra. Spishi nyingine za familia hii zinatambulika kama magugu sehemu mbali mbali duniani zikiwemo: Cytisus scoparius, Robinia pseudoacacia, Ulex europaeus, Pueraria montana, na baadhi ya spishi za jenasi Lupinus.

Maana na chanzo cha jina

[hariri | hariri chanzo]

Jina 'Fabaceae' linatokana na jenasi ya zamani Faba ambayo kwa sasa ipo ndani ya jenasi Vicia. Neno "faba" linatoka kwenye kilatini, maana yake nyepesi ikiwa ni "haragwe". Leguminosae ni jina la zamani ambalo bado linakubalika ambalo linaelezea tunda la mimea ya familia hii, ambayo inaitwa legumes kwa jina la kiingereza.

Uainishaji wa kisayansi

[hariri | hariri chanzo]

Fabaceae imewekwa katika oda ya Fabales kulingana na mifumo mingi ya uainishaji, ukiwemo mfumo wa APG III. Kwa sasa, familia hii inajumuisha nusufamilia sita: [11]

Mimea ya familia ya Fabaceae ipo kwenye makundi mbali mbali kuanzia miti mikubwa (kama Koompassia excelsa) au mimea ya majani ya msimu. Hata hivyo mimeo mingi kwenye familia hii ipo kwenye kundi la mimea ya kudumu isiyo ya miti. Maua ya mimea ya familia hii hua madogo kwenye mfumo wa inflorescences japo wakati wingine ua hubaki moja. Uchavushaji wa maua yake huzaa matunda aina ya mikunde.

Familia ya Fabaceae ina aina nyingi tofauti za ukuaji, zikiwemo, kama miti, vichaka au mimea ya kutambaa na kupanda. Mimea ya familia hii isiyo ya miti inaweza kua ya msimu au muda mrefu, bila mkusanyiko wa majani ya chini au mwisho. Mimea mingi ya jamii ya mikunde ina kamba kamba (tendrils) ambazo husaidia mmea kushishikiza. Inaweza kusimama wima yenyewe, kukua juu ya mimea mingine (epiphytic) au kutanda/kutambaa. Ile inayotambaa hua inajishikilia kwa matawi yake au kamba kamba (tendrils). Mimea ya jamii hii inaweza kua ambayo inaweza kuvumilia ukame, inayopenda maji au ile inayoweza kuishi mazingira mengi. [13][14]

 1. Christenhusz, M. J. M.; Byng, J. W. (2016). "The number of known plants species in the world and its annual increase". Phytotaxa. 261 (3): 201–217. doi:10.11646/phytotaxa.261.3.1.
 2. Stevens, P. F. "Fabaceae". Angiosperm Phylogeny Website. Version 7 May 2006. Iliwekwa mnamo 28 Aprili 2008.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
 3. Magallón, S. A., and Sanderson, M. J.; Sanderson (2001). "Absolute diversification rates in angiosperm clades" (PDF). Evolution. 55 (9): 1762–1780. doi:10.1111/j.0014-3820.2001.tb00826.x. PMID 11681732. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 19 Oktoba 2013.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: multiple names: authors list (link)
 4. Burnham, R. J.; Johnson, K. R. (2004). "South American palaeobotany and the origins of neotropical rainforests". Philosophical Transactions of the Royal Society B: Biological Sciences. 359 (1450): 1595–1610. doi:10.1098/rstb.2004.1531. PMC 1693437. PMID 15519975.
 5. Lewis G., Schrire B., Mackinder B. and Lock M. 2005. (eds.) Legumes of the world. The Royal Botanic Gardens, Kew, Reino Unido. 577 pages. 2005. ISBN|1-900347-80-6
 6. Doyle, J. J., J. A. Chappill, C.D. Bailey, & T. Kajita. 2000. Towards a comprehensive phylogeny of legumes: evidence from rbcL sequences and non-molecular data. pp. 1 -20 in Advances in legume systematics, part 9, (P. S. Herendeen and A. Bruneau, eds.). Royal Botanic Gardens, Kew, UK.
 7. Kajita, T.; Ohashi, H.; Tateishi, Y.; Bailey, C. D.; Doyle, J. J. (2001). "rbcL and legume phylogeny, with particular reference to Phaseoleae, Millettieae, and allies". Systematic Botany. 26 (3): 515–536. doi:10.1043/0363-6445-26.3.515 (si hai 25 Februari 2021). JSTOR 3093979.{{cite journal}}: CS1 maint: DOI inactive as of 2021 (link) CS1 maint: date auto-translated (link)
 8. Wojciechowski, M. F., M. Lavin and M. J. Sanderson; Lavin; Sanderson (2004). "A phylogeny of legumes (Leguminosae) based on analysis of the plastid matK gene resolves many well-supported sub clades within the family". American Journal of Botany. 91 (11): 1846–1862. doi:10.3732/ajb.91.11.1846. PMID 21652332. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-06-21. Iliwekwa mnamo 2021-04-21. {{cite journal}}: Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link)
 9. Angiosperm Phylogeny Group [APG] (2003). "An update of the Angiosperm Phylogeny Group classification for the orders and families of flowering plants: APG II" (PDF). Botanical Journal of the Linnean Society. 141 (4): 399–436. doi:10.1046/j.1095-8339.2003.t01-1-00158.x. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2018-03-10. Iliwekwa mnamo 2021-04-21. {{cite journal}}: Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help)
 10. Burkart, A. Leguminosas. In: Dimitri, M. 1987. Enciclopedia Argentina de Agricultura y Jardinería. Tomo I. Descripción de plantas cultivadas. Editorial ACME S.A.C.I., Buenos Aires. pages: 467-538
 11. The Legume Phylogeny Working Group (LPWG). (2017). "A new subfamily classification of the Leguminosae based on a taxonomically comprehensive phylogeny". Taxon. 66 (1): 44–77. doi:10.12705/661.3.
 12. NOTE: The subfamilial name Papilionoideae for Faboideae is approved by the International Code of Nomenclature for algae, fungi, and plants, Article 19.8
 13. Watson L.; Dallwitz, M. J. (2007-06-01). "Familia za mimea inayotoa maua: Leguminosae". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-10-08. Iliwekwa mnamo 25 Agosti 2021. {{cite web}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
 14. Judd, Walter S; Campbell, Christopher S; Kellogg, Elizabeth A; Stevens, Peter F; Donoghue, Michael J (2002). Plant Systematics: A Phylogenetic Approach. London: Sinauer Associates. uk. 287-292. ISBN 9781605353890.