Benedikto wa Aniane

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Benedikto wa Aniane.

Benedikto wa Aniane, O.S.B. (jina la kuzaliwa Witiza; huitwa pengine Benedikto wa pili; 747 hivi – 12 Februari 821) alikuwa mmonaki na mrekebishaji wa Utawa wa Mt. Benedikto, ambaye aliathiri sana hali ya Kanisa katika dola la Karolo Mkuu pia kwa kurekebisha liturujia ya Roma.

Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa kila mwaka siku ya kifo chake[1].

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Kadiri ya Ardo Smaragdus, aliyewahi kuandika maisha ya Benedikto, yeye alikuwa mtoto wa Aigulf, mtawala wa Kigoti wa Maguelonne mwaka 752. Jina lake la kikabila lilikuwa Witiza.

Alilelewa katika ikulu ya mfalme wa Wafaranki ya Pipino Mfupi, akaingia utumishi wake, halafu akamtumikia Karolo Mkuu, akishiriki kampeni yake nchini Italia mwaka 773, ambapo alinusurika kufa maji katika mto Ticino karibu Pavia wakati wa kujaribu kuokoa askari mwenzake.

Baadaye aliacha ikulu awe mtawa katika monasteri ya Saint-Seine.

Mwaka 780 hivi, alianzisha jumuia iliyofuata umonaki wa mashariki huko Aniane, Languedoc, lakini haikustawi.

Basi, mwaka 782 alianzisha hukohuko monasteri nyingine ikifuata Kanuni ya Mt. Benedikto, ambayo ilistawi na kumwezesha kuanzisha au kurekebisha monasteri kadhaa, na hatimaye kuwa kama abati wa monasteri zote wa dola la Karolo Mkuu.[2]

Alikuwa mwenyekiti wa halmashauri ya maabati ambayo mwaka 817 huko Aachen ilitunga "Codex regularum", yaani mkusanyo wa taratibu za kufuatwa katika jumuia zao zote.

Baadaye kidogo, aliandika "Concordia regularum", yaani ulinganifu wa kanuni 27 tofauti.

Vitabu hivyo viwili viliathiri moja kwa moja umonaki wa magharibi.

Benedikto alifariki huko Kornelimünster Abbey, monasteri ambayo mfalme Luis Mtawa alikuwa amemjengea aweze kusimamia urekebisho wake wote.

Maandishi[hariri | hariri chanzo]

Ya hakika[hariri | hariri chanzo]

  • Codex regularum monasticarum et canonicarum in Patrologia Latina, CIII, 393-702;
  • Concordia regularum, PL 103:393-702
  • Barua, PL 103:703-1380.

Ya shaka[hariri | hariri chanzo]

Maandishi mengine (yaliyomo PL 103:1381ff) hayaaminika kuwa ya kwake kweli.

  • Ardo Smaragdus, Life, op. cit., CIII, 353 sqq.;
  • Monumenta Germaniae Historica: Script., XV, I, 200-220;
  • Acta Sanctorum, Feb., II, 606 sqq.;
  • NICOLAI, Der hl. Benedict, Gründer von Aniane und Cornelimünster (Cologne, 1865);
  • PAULINIER, S. Benoit d'Aniane et la fondation du monastere de ce nom (Montpellier, 1871);
  • FOSS, Benedikt von Aniane (Berlin, 1884);
  • PUCKERT, Aniane und Gellone (Leipzig, 1899);
  • HAUCK, Kirchengesch. Deutschlands (2nd ed., Leipzig, 1900), II, 575 sqq.;
  • BUTLER, Lives of the Saints, 12 Feb.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Martyrologium Romanum
  2. Attwater, Donald and Catherine Rachel John. The Penguin Dictionary of Saints. 3rd edition. New York: Penguin Books, 1993. ISBN 0-14-051312-4.

Maandishi yake[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.