Nenda kwa yaliyomo

Babati Mjini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Babati (mji))


Babati
Babati is located in Tanzania
Babati
Babati

Mahali pa mji wa Babati katika Tanzania

Majiranukta: 4°13′12″S 35°45′0″E / 4.22000°S 35.75000°E / -4.22000; 35.75000
Nchi Tanzania
Mkoa Manyara
Wilaya Wilaya ya Babati Mjini
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 129,572
Ziwa Babati na Mlima Kwaraa kando la mji wa Babati

Babati ni mji mdogo wenye halmashauri na hivyo hadhi ya wilaya katika Mkoa wa Manyara nchini Tanzania yenye postikodi namba 27100.

Ni pia makao makuu ya Mkoa wa Manyara, takriban kilomita 170 kusini mwa Arusha na kilomita 220 upande wa kaskazini wa Dodoma. Mji uko karibu na Hifadhi ya Tarangire ukienea kati ya ncha ya kaskazini ya Ziwa la Babati na karibu na tako la Mlima Kwaraha (m 2145 juu ya UB).

Hadi mwaka 2012 kata za mji wa Babati zilikuwa sehemu ya Wilaya ya Babati ya awali; baadaye Babati Mjini na Wilaya ya Babati Vijijini zilitengwa kuwa halmashauri mbili za pekee.

Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, wilaya ya Babati mjini ilikuwa na wakazi wapatao 93,108 waishio humo. Katika sensa ya mwaka 2022 wazazi walihesabiwa 129,572 [1].

Kata iliyo kitovu cha mji huitwa pia "Babati" ikiwa na wakazi 21,618 [2].

Babati iliendelea kiasi kutokana na kukaa kando ya barabara kuu kati ya Dodoma na Arusha. Hata hivyo ilikuwa kama kijiji kikubwa tu hadi kuwa makao makuu ya Wilaya ya Babati iliyoanzishwa mwaka 1985. Tangu siku zile iliendelea kukua haraka hadi kupata halmashauri yake kama mji na kuwa mji mkuu wa mkoa mpya mwaka 2012.

Tangu kutengenezwa kwa barabara kuu watalii wameanza kufika Babati.

Asili ya jina Babati

[hariri | hariri chanzo]

Kuna hadithi inayosimuliwa asili ya jina. Zamani za ukoloni wa Kijerumani barabara ilijengwa karibu na mahali pa Babati ya leo. Msimamizi Mjerumani akamwauliza kijana mwenyeji jina la mahali, lakini kijana hakumwelewa akafikiri huyu mgeni aliuliza, eti babake ni nani. Hivyo akamjibu kwa lugha ya Kigorowa "baba ti" inayomaanisha "baba ni huyu" akimdokezea mzee aliyekaa karibu. Mjerumani alifikiri hilo ni jina akaliandika likabaki hadi leo.[3]

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
Kata za Wilaya ya Babati Mjini - Mkoa wa Manyara - Tanzania

Babati | Bagara | Bonga | Maisaka | Mutuka | Nangara | Sigino | Singe


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Manyara bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Babati Mjini kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.