Alexey Vasilyev
Alexey Mikhailovich Vasilyev (kwa Kirusi Алексей Михайлович Васильев; amezaliwa tarehe 26 Aprili 1939 mjini Leningrad) ni mwanasayansi wa Umoja wa Kisovyeti na Urusi, daktari wa historia, profesa na mwanachama wa Chuo cha Sayansi cha Urusi.
Wasifu
[hariri | hariri chanzo]Mwaka 1956 alijiunga na Chuo Kikuu cha Moscow cha Mahusiano ya Kimataifa cha Wizara ya Mambo ya Nje ya Umoja wa Kisovyeti (MGIMO). Miaka 1960-1961 alikuwa na mazoea kwenye Chuo Kikuu cha Kairo huko Misri. Kuanzia mwaka 1962 hadi mwaka 1967 alifanya kazi kama msaidizi wa mchambuzi wa kisiasa wa gazeti la Pravda (Ukweli kwa Kiswahili) Victor Mayevsky (1921-1976).
Mwaka 1966 alihitimu katika uzamivu wa Taasisi ya Mafunzo ya Mashariki ya Chuo cha Sayansi cha Umoja wa Kisovyeti akitetea tasnifu ambayo mada yake ni Harakati ya Wahhabiya na dola la kwanza la Wasaud Uarabuni mnamo karne ya 18[1][2].
Mwaka 1967 alitumwa nchini Vietnam kama mwandishi mwenyewe wa habari wa kijeshi wa gazeti la Pravda. Miaka 1969-1971 alibaki katika nafasi hiyo huku akifanya uhariri. Mara nyingi alikwenda kwenye sehemu zenye mizozo mikali apate habari.
Tangu mwaka 1971 hadi mwaka 1975 alikuwa mwandishi mwenyewe wa habari wa gazeti la Pravda mjini Ankara na kutoa habari juu ya Uturuki, Iran, Afghanistan, Syria na mataifa ya Uarabuni pamoja na Vita kati ya Waisraeli na Waarabu ya mwaka 1973. Miaka 1975-1979 alikuwa mwandishi wa habari wa Pravda huko Misri, Sudan, Libya, Yemen na Ethiopia.
Kuanzia mwaka 1979 hadi mwaka 1983 alikuwa mchambuzi wa Idara ya Masuala ya Kimataifa ya gazeti la Pravda.
Mwaka 1981 alitetea tasnifu ya udaktari ya Maendeleo ya muundo wa kijamii na kisiasa wa Saudia miaka 1745-1973 katika Taasisi ya Mafunzo ya Mashariki[3].
Tangu mwaka 1983 hadi mwaka 1992 alikuwa Naibu Mkurugenzi wa Taasisi ya Afrika ya Chuo cha Sayansi cha Umoja wa Kisovyeti / Urusi. Miaka 1992-2015 aliongoza Taasisi hiyo na baadaye mwaka 2015 akawa Rais Mheshimiwa wa Taasisi ya Afrika.
Kuanzia mwaka 2003 anaongoza Idara ya Mafunzo ya Kiafrika na Kiarabu ya Chuo Kikuu cha Urusi cha Urafiki wa Watu (RUDN).
Ameoa na ana mabinti wawili pamoja na wajukuu watatu wa kike.
Shughuli za kisayansi
[hariri | hariri chanzo]Fani yake inajumuisha masuala ya kimsingi ya historia ya kijamii na kisiasa ya nchi za Kiarabu wakati wa Zama Mpya, mahusiano ya kimataifa ya nchi za Mashariki ya Kati ikiwemo ni uhusiano na Urusi, maana ya dini katika mapambano ya kisiasa, mabadiliko ya kijamii katika Kanda ya Mashariki ya Kati, mambo ya kikabila na kisaikolojia ya umma pamoja na itikadi kali na ugaidi.
Bw. Vasilyev alikuwa wa kwanza nchini Umoja wa Kisovyeti aliyetafiti harakati ya Wahhabiya akijali maandishi ya mwanzilishi wake Muhammad ibn Abd al-Wahhab na watangulizi wake. Kitabu kikuu cha Vasilyev ni Historia ya Saudia kilichochapishwa mara nyingi katika Kirusi, Kiarabu na Kiingereza. Alichungua maendeleo ya kijamii, kiuchumi na ya kisiasa ya nchi hiyo ya karne 2 na nusu akitumia vyanzo vya Kiarabu, Kituruki, Kiingereza, Kifaransa, Kiitalia, Kijerumani na Kirusi, ikiwemo vile vya nyaraka za Umoja wa Kisovyeti na Urusi. Zaidi ya hayo aliandika vitabu 2 vinavyohusu Saudia. Kitabu chake cha mwisho kiitwacho Mfalme Faisal, nafsi, enzi, imani kiliheshimwa na jukumu la mtu huyo katika maisha na siasa ya Saudia, maana kubwa ya dini na imani katika kuundwa kwa sera ya kisiasa ya nchi.
Bw. Vasiliev alikuwa mjumbe binafsi wa Rais wa Shirikisho la Urusi wa Mahusiano na Viongozi wa Mataifa ya Afrika[4]. Alikuwepo katika ujumbe wa Urusi wa mikutano ya kilele ya G8 na ujumbe wa Rais Mikhail Gorbachov, Dmitry Medvedev, Waziri Mkuu Viktor Chernomyrdin. Anashiriki katika makongamano mbalimbali ya kimataifa ikiwemo yale yaliyoendeshwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO). Yeye pia ni mwanachama wa Harakati ya Pugwash nchini Urusi.
Tuzo na heshima
[hariri | hariri chanzo]- Mwanasayansi mstahiki wa Shirikisho la Urusi (1999)[5]
- Tuzo ya E. V. Tarle ya Chuo cha Sayansi cha Urusi (2003) kwa ajili ya maandishi yake ya historia ya kijamii na kisiasa ya nchi za Mashariki ya Kati
- Nishani ya Heshima (2009)[6]
- Nishani ya Urafiki (2011) kwa ajili ya mchango mkubwa katika maendeleo na kuimarishwa kwa mahusiano kati ya Shirikisho la Urusi na mataifa ya Afrika[7]
- medali kadhaa
Maandishi makuu
[hariri | hariri chanzo]- Нефть: монополии и народы. — М.: 1964.
- Монополии и народы. (на болг. языке). София: 1965.
- Пуритане ислама? Ваххабизм и первое государство Саудидов в Аравии, (1744/45-1818). — М.: 1967.
- Ракеты над цветком лотоса: Вьетнам в дни войны. — M.: 1970.
- Путешествие в «Арабиа Феликс». — М.: 1974.
- Факелы Персидского залива. — М.: 1976.
- Факелы Персидского залива. (на фарси). — Тегеран, 1358.
- Трудный перевал. — М., 1977.
- Мост через Босфор. — М., 1979.
- Мост через Босфор. — 2-е изд., перераб. и доп. — М.: 1989.
- Нефть залива и арабская проблема. (на араб. языке). — Каир:. 1979.
- История Саудовской Аравии (1745—1973). — М.: 1982.
- История Саудовской Аравии — [Изд. испр. и доп.] (на араб. языке). — М.: 1986.
- Библиография Саудовской Аравии. — М.: 1983.
- Персидский залив в эпицентре бури. — М., 1983.
- Персидский залив в эпицентре бури. (на арм. языке) — Ереван: 1986.
- Персидский залив под прицелом Пентагона. (на араб. языке). — М.: 1984.
- Египет и египтяне. — М., 1986.
- Египет и египтяне. (на араб. языке) — М., 1989.
- Египет и египтяне. (на латыш. языке). — Рига: 1990.
- Египет и египтяне. (на эст. языке). — Таллинн: 1992.
- Египет и египтяне. — 2-е изд., испр. и доп. (на араб. языке) — Бейрут: 1994.
- Египет и египтяне. — 3-е изд., перераб. и доп. — М.: 2008.
- Корни тамариска. — М., 1987.
- Россия на Ближнем и Среднем Востоке: от мессианства к прагматизму. — М., 1993.
- Russian Policy in the Middle East: From Messianism to Pragmatism. — Reading: 1993.
- Россия на Ближнем и Среднем Востоке: от мессианства к прагматизму. (на араб. языке). — Каир: 1996.
- История Саудовской Аравии от середины XVIII в. до конца XX в. — М., 1994.
- История Саудовской Аравии от середины XVIII в. до конца XX в. (на араб. языке). — Бейрут: 1995.
- The History оf Saudi Arabia. — London: 1998.
- История Саудовской Аравии (1745 — конец XX в.). — М., 1999.
- Аннотированная библиография Саудовской Аравии (Публикации на русском языке). — М., 2000.
- Иракская агрессия против Кувейте. в зеркале российской прессы (август 1990 — апрель 1991). — М., 2000.
- Приватизация: Сравнительный анализ: Россия, Центральная Азия, арабские страны (в соавторстве с Кукушкиным В. Ю., Ткаченко А. А.). — М.: 2002.
- Африка — падчерица глобализации. — М., 2003.
- Ближневосточный конфликт: состояние и пути урегулирования (в соавторстве с Ткаченко А. А. и др.). — М.: 2007
- Король Фейсал. Личность. Эпоха. Вера. — М., 2010. ISBN 978-5-02-036408-0
- Король Фейсал. Личность. Эпоха. Вера. (на араб. языке). — Бейрут, 2012. ISBN 978-1-85516-862-6
- King Faisal of Saudi Arabia. Personality, Faith and Times. — London, 2012. ISBN 978-0-86356-689-9
- Рецепты арабской весны. — М.: Алгоритм, 2012. ISBN 978-5-4438-0148-3
- Африка и вызовы XXI в. — М., 2012. ISBN 978-5-02-036501-8
- Исламские радикальные движения на политической карте современного мира. Вып. 2. Северный и Южный Кавказ (в соавт.). — М., 2017. ISBN 978-5-7164-0719-0
- Исламистские движения на политической карте современного мира. Вып. 3. Афроазиатская зона нестабильности (в соавт.). — М., 2018. ISBN 978-5-91298-219-4
- От Ленина до Путина. Россия на Ближнем и Среднем Востоке. — М., 2018. ISBN 978-5-227-07511-6
- Russian Middle East Policy. From Lenin to Putin. — London, 2018. ISBN 978-1-138-56360-5 (hard cover). ISBN: 978-1-315-12182-6 (e-book)
Tafsiri
[hariri | hariri chanzo]- ن لينين إلى بوتين. روسيا في الشرق الأوسط والشرق الأدنى | فاسيليف أليكسي | [Пер. на араб. М. Н. Эльгебали] — Каир: Издательство «Российские новости», 2018. — 746 с.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Васильев, Алексей Михайлович. Ваххабизм и первое государство Саудидов в Аравии (1744/45-1818 гг.): Автореф. дис. ... канд. ист. наук / АН СССР. Ин-т народов Азии. - Москва: [б. и.], 1966. — 16 с.
- ↑ Известия. Ру
- ↑ Васильев, Алексей Михайлович. Эволюция социально-политической структуры Саудовской Аравии, 1745-1973 гг.: дисс. ... д-ра ист. наук: 07.00.03. — Москва, 1980. — 420 с.
- ↑ "Распоряжение Президента Российской Федерации от 20.02.2006 г. № 78-рп «О специальном представителе Президента Российской Федерации по связям с лидерами африканских государств»". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-01-13. Iliwekwa mnamo 2019-01-12.
{{cite web}}
: no-break space character in|title=
at position 59 (help) - ↑ Указ Президента Российской Федерации от 4 июня 1999 № 701 «О награждении государственными наградами Российской Федерации работников Российской академии наук»
- ↑ Указ Президента Российской Федерации от 18 августа 2009 № 941 «О награждении государственными наградами Российской Федерации»
- ↑ "Указ Президента Российской Федерации от 20 марта 2011 года № 328 «О награждении орденом Дружбы Васильева А. М.»". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-07-05. Iliwekwa mnamo 2015-07-04.
{{cite web}}
: no-break space character in|title=
at position 61 (help)
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Bw. Vasilyev katika tovuti rasmi ya Chuo cha Sayansi cha Urusi
- Wasifu wake kwenye tovuti ya Taasisi ya Afrika
- Makala juu yake katika Baraza la Masuala ya Kimataifa ya Urusi
- Alexey Vasilyev
- Habari katika tovuti ya nyaraka za Chuo cha Sayansi cha Urusi
- Alexey Vasilyev (miaka 70 tangu kuzaliwa kwake)
- Marejeo ya vitabu vyake