Nenda kwa yaliyomo

Vita vya Yom Kippur

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kuvuka daraja katika vita vya Yom Kippur.

Vita vya Yom Kippur (pia: Vita vya Ramadan, Vita vya Oktoba; kwa Kiyahudi: מלחמת יום הכיפורים‎, Milẖemet Yom HaKipurim, au מלחמת יום כיפור, Milẖemet Yom Kipur; kwa Kiarabu: حرب أكتوبر‎, Ḥarb ʾUktōbar, au حرب تشرين, Ḥarb Tišrīn) ni vita kati ya Waisraeli na Waarabu vya mwaka 1973.

Vita vya Yom Kippur vilikuwa mashambulio ya Misri na Syria dhidi ya Israeli katika mwezi Oktoba 1973. Mashambulio yalianza kwenye sikukuu ya Kiyahudi ya Yom Kippur. Jeshi la Misri lilifaulu kuingia kwenye rasi ya Sinai na Syria kwenye milima ya Golan. Lakini Syria ilirudishwa nyuma haraka na Waisraeli walifikia kilomita 40 tu kutoka Dameski. Jeshi la Misri lilishindwa zaidi hadi Israeli iliweza kuvuka mfereji wa Suez na kufunga kikosi kikubwa cha Wamisri nyuma ya mstari wa mapigano na kuingia katika mji wa Suez na hata kukaribia Kairo. Mnamo 23 Oktoba pande zote zilikubali kusimamisha mapigano kwa ombi la UM. Baada ya majadiliano marefu, kila upande ulirudisha wanajeshi wake kilomita kadhaa kwa kusudi la kuwa na umbali kati ya majeshi.

Misri na Israeli zikaendelea kuwa na majadiliano na kupatana kufanya amani mwaka 1978. Israeli iliondoka katika Sinai na nchi zote mbili zikafungua ubalozi katika nchi ya pili. Ukanda wa Gaza ulibaki chini ya Israeli.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Vita vya Yom Kippur kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.