Suez

Majiranukta: 29°58′N 32°33′E / 29.967°N 32.550°E / 29.967; 32.550
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bandari na chanzo cha mfereji mjini Suez

Suez (ar. السويس as-Suways) ni mji na bandari nchini Misri. Iko kwenye mwambao wa kaskazini wa ghuba ya Suez au kwa lugha nyingine kwenye upande wa kusini wa Mfereji wa Suez. Mwaka 2012 mji ulikuwa na wakazi 565,716.

Suez iko takriban kilomita 135 upande wa mashariki ya Kairo kwenye shingo ya nchi ambako umbali na Bahari ya Mediteranea haifikii kilomita 150. Kwa sababu hii Suez ilikuwa mahali palipofaa kwa biashara na masoko ya biashara kati ya Mediteranea na Bahari Hindi. Tangu kubuniwa kwa njia ya bahari kutoka Ulaya kwenda Uhindi kupitia Rasi ya Tumaini Njema (Afrika Kusini) biashara hii ilififia. Hata hivyo Suez iliendelea kuwa bandari ya maana kwa wasafiri Waislamu walioelekea Makka kwa hajj.

Umuhimu wa Suez ulirudishwa na kuongezwa tangu kujengwa kwa Mfereji wa Suez tarehe 17 Novemba 1869. Sehemu kubwa ya biashara ya dunia kwa meli ilipita kwenye mfereji na bandari ya Suez.

Suez imeendelea kuwa mji muhimu wa viwanda pamoja na viwanda vya kusafisha mafuta, vya kemia na feleji.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

29°58′N 32°33′E / 29.967°N 32.550°E / 29.967; 32.550