Aleksanda I wa Aleksandria

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Aleksanda wa Aleksandria)
Jump to navigation Jump to search

Aleksanda I wa Aleksandria (alifariki tarehe 26 Februari[1] au 17 Aprili, 326 au 328) alikuwa Patriarki wa 19 wa Aleksandria, Misri. Wakati wa uongozi wake alikabili masuala mbalimbali, kama vile tarehe ya Pasaka, matendo ya Meletius wa Lycopolis, na hasa Uario. Ndiye aliyekuwa mpinzani mkuu wa padri Ario na wa mafundisho yake hadi Mtaguso wa kwanza wa Nisea. Ndiye aliyemuandaa shemasi Atanasi wa Aleksandria kuwa mwandamizi wake.[2]

Tangu kale anaheshimiwa na Waorthodoksi wa Mashariki, Waorthodoksi na Wakatoliki kama mtakatifu[3].

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 26 Februari au 29 Mei[4].

Maandishi[hariri | hariri chanzo]

Mengi kati ya maandishi yake hayakutufikia, isipokuwa barua mbili. Mengine hayana hakika.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Alexander I (313–328). Official web site of the Greek Orthodox Patriarchate of Alexandria and All Africa. Iliwekwa mnamo 2011-02-08.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Christian cross.svg Makala hii kuhusu Mkristo huyu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Aleksanda I wa Aleksandria kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.