Nenda kwa yaliyomo

Aleksanda I wa Aleksandria

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha takatifu katika monasteri Veljusa , Masedonia.

Aleksanda I wa Aleksandria (alifariki tarehe 26 Februari[1] au 17 Aprili, 326 au 328) alikuwa Patriarki wa 19 wa Aleksandria, Misri, maarufu kwa imani na juhudi.

Wakati wa uongozi wake alikabili masuala mbalimbali, kama vile tarehe ya Pasaka, matendo ya Meletius wa Lycopolis, na hasa Uario. Ndiye aliyekuwa mpinzani mkuu wa padri Ario na wa mafundisho yake hadi Mtaguso wa kwanza wa Nisea, ambao aliushiriki uzeeni pamoja na maaskofu wengine 317 na ambao ulikataa uzushi huo hata kwa kutunga kanuni ya imani sahihi. Ndiye aliyemuandaa shemasi Atanasi wa Aleksandria kuwa mwandamizi wake.[2]

Tangu kale anaheshimiwa na Waorthodoksi wa Mashariki, Waorthodoksi na Wakatoliki kama mtakatifu[3].

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 26 Februari[4] au 29 Mei[5].

Maandishi[hariri | hariri chanzo]

Mengi kati ya maandishi yake hayakutufikia, isipokuwa barua mbili. Mengine hayana hakika.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. http://saints.sqpn.com/saint-alexander-of-alexandria/
  2. Christie, Albany James (1867). "Alexander of Alexandria". In William Smith. Dictionary of Greek and Roman Biography and Mythology. 1. Boston: Little, Brown and Company. pp. 111–112. http://www.ancientlibrary.com/smith-bio/0120.html. Archived 30 Machi 2009 at the Wayback Machine. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-03-30. Iliwekwa mnamo 2017-02-10.
  3.  Campbell, Thomas Joseph (1913). "St. Alexander (of Alexandria)". Catholic Encyclopedia. New York: Robert Appleton Company.
  4. Martyrologium Romanum
  5. https://catholicsaints.info/saint-alexander-of-alexandria/

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • "Alexander I (313–328)". Official web site of the Greek Orthodox Patriarchate of Alexandria and All Africa. Iliwekwa mnamo 2011-02-08.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.