Albano Roe

Albano Roe, O.S.B. (Bury St. Edmunds, Suffolk, Uingereza, 20 Julai 1583 – Tyburn, London, 21 Januari 1642) alikuwa Mkristo wa Kanisa la Anglikana kabla hajajiunga na Kanisa Katoliki pamoja na ndugu yake James.
Baada ya kuhamia Ufaransa, aliingia seminari (1607) kwa kengo la kurudi kwao kufanya uchungaji usioruhusiwa na serikali, lakini alifukuzwa kwa tabia yake (1610). Baadaye alijiunga na monasteri ya Wabenedikto (1613) na kupewa daraja ya upadri (1615).
Hapo alirudi London lakini alifukuzwa baada ya muda mfupi. Alirudi tena mwaka 1618 akafungwa hadi 1623. Miaka miwili baadaye akarudi tena akafungwa kwa miaka 17, lakini gereza halikuwa na nidhamu kali, hivyo akaweza kufanya utume wake mchana na kurudi kulala jela usiku.
Mwaka 1641 alihamishiwa gereza lingine alipokataa kuasi na kwa ajili hiyo mwaka uliofuata aliuawa kwa kunyongwa chini ya sheria [1].
Papa Paulo VI tarehe 25 Oktoba 1970 alimtangaza kuwa mtakatifu mfiadini pamoja na wenzake 39.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Mabradha wa Shule za Kikristo
- Orodha ya Watakatifu Waaugustino
- Orodha ya Watakatifu Wabazili
- Orodha ya Watakatifu Wabenedikto
- Orodha ya Watakatifu Wadominiko
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
- Orodha ya Watakatifu Wajesuiti
- Orodha ya Watakatifu Wakarmeli
- Orodha ya Watakatifu Wakolumbani
- Orodha ya Watakatifu Wamersedari
- Orodha ya Watakatifu Waoratori
- Orodha ya Watakatifu Wapasionisti
- Orodha ya Watakatifu Wapremontree
- Orodha ya Watakatifu Waredentori
- Orodha ya Watakatifu Wasalesiani
- Orodha ya Watakatifu Waskolopi
- Orodha ya Watakatifu Wateatini
- Orodha ya Watakatifu Watrinitari
- Orodha ya Watakatifu Watumishi wa Maria
- Orodha ya Watakatifu Wavinsenti
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Story of Saint Alban Roe Ilihifadhiwa 16 Februari 2018 kwenye Wayback Machine. on Ampleforth's website
. Catholic Encyclopedia. New York: Robert Appleton Company. 1913.- Patron Saints Index: Saint Alban Bartholomew Roe
| Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |