Adama Barrow

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Adama Barrow (2016)

Adama Barrow (*16 Februari 1965) ni rais wa Gambia na mwanasiasa wa chama cha United Democratic Party.[1]

Utoto na shule[hariri | hariri chanzo]

Barrow alizaliwa katika kijiji cha Mankamang Kunda karibu na Basse. Alisoma shule ya msingi Koba Kunda halafu sekondari ya Crab Island mjini Banjul. Baadaye alipata nafasi kwenye Muslim High School ya Banjul.

Kazi[hariri | hariri chanzo]

Baada ya kufaulu aliajiriwa na kampuni ya Alhagie Musa & Sons akapandishwa cheo hadi kuwa muuzaji mkuu.[2]

Baada ya mwaka 2000 Barrow alihamia London aliposoma uchumi. Wakati huu alifanya kazi ya usiku kama mlinzi wa nyumba kwa kujipatia riziki. [3]

Baada ya kurudi Gambia aliunda mwaka 2006 kampuni ya Majum Real Estate akawa meneja mkuu hadi sasa.[2]

Siasa[hariri | hariri chanzo]

Mwaka 2016 Barrow alichaguliwa kuwa mgombea wa urais wa pamoja katika mkutano wa vyama 7 vya upinzani. [4][5]

Tarehe 2 Desemba 2016 Barrow alishtusha taifa kwa kumshinda Yammeh katika uchaguzi wa urais [6][7] kwa kupata kura 263,000 au asilimia 45 za kura zote dhidi ya kura 212,000 au asilimia 36 kwa rais Yahya Jammeh. Mgombea wa tatu Mama Kandeh alipata asilimia 17.

Kwanza Rais Yahya Jammeh alikubali kushindwa hata kabla ya tangazo rasmi la matokeo[8][9], lakini siku nane baadaye alianza kung'ang'ania madaraka.

Kufuatana na katiba rais Adama Barrows alitakiwa kuapishwa takriban siku 60 baada ya uchaguzi.[10], lakini 9 Disemba 2016 rais Jammeh alitangaza ya kwamba hakubali matokeo akitaka uchaguzi mpya.[11]

Tarehe 19 Januari 2017, rais mteule aliapishwa katika ubalozi wa Gambia huko Dakar, halafu wanajeshi wa Senegal, Nigeria na Ghana walivamia nchi ili kumuondoa madarakani kwa idhini ya Umoja wa Mataifa.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

 1. "Breaking News: Adama Barrow Is UDP’s Candidate", 2016-09-01. (en-GB) 
 2. 2.0 2.1 Who Is Adama Barrow? (1 September 2016). Iliwekwa mnamo 2 December 2016.
 3. "Argos guard tackles Gambia strongman", 2016-11-20. (en-GB) 
 4. Mowat. "North London Argos worker takes on hardline Islamist in bid to be next president of GAMBIA". 
 5. Yaya Barry, Jaime. "Gambia’s Leader Vowed to Rule for a Billion Years. A Vote Will Test That.", New York Times, 30 November 2016. 
 6. Barrow ambwaga Jammeh urais Gambia, Tovuti ya Idhaa ya Kiswahili, Sauti ya Ujerumani, imeangaliwa 3 Desemba 2016
 7. Gambia's Yahya Jammeh loses election to Adama Barrow (2 December 2016).
 8. Adama Barrow ashinda urais nchini Gambia, Rais Jammeh akubali kushindwa, tovuti ya Sauti ya Ufaransa, imeangaliwa 3. Desemba 2016
 9. "The Gambia’s President Jammeh to concede defeat in election", The Guardian, 2 December 2016. 
 10. Gambia 2016: Defeated Jammeh To Address The Nation. Jalada kutoka ya awali juu ya 2016-12-03. Iliwekwa mnamo 2016-12-03.
 11. Gambia: troops deployed to streets as president rejects election defeat theguardian.com 10-12-2016, imeangaliwa 10-12-2016