Nenda kwa yaliyomo

Utitiri (Arithropodi)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Acarina)
Utitiri
Kifani cha utitiri mwekundu wa kuku
Kifani cha utitiri mwekundu wa kuku
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia
Faila: Arthropoda
Nusufaila: Chelicerata
Ngeli: Arachnida
Nusungeli: Acari
Ngazi za chini

Oda za juu 3 na oda 6:

Kwa asili jina utitiri hutumika kwa ugonjwa wa kuku ambao unasababishwa na wadudu wadogo walio na mnasaba na kupe na papasi. Lakini kwa sababu hakuna jina la jumla la Kiswahili kwa kundi la Acari “utitiri” hutumika zaidi na zaidi kwa spishi nyingine za Acari. Kwa asili pia neno hili lilikuwa nomino isiyoweza kuhesabiwa, kama sukari kwa mfano, lakini watu wengine wameanza kulichukulia kama neno katika umoja (pengine hata titiri) na "matitiri" kama wingi. Utitiri ni nusungeli katika ngeli ya Arachnida. Kwa hivyo wana miguu minane kama buibui na nge.

Utitiri ni arithropodi wadogo. Spishi kubwa kabisa zina mm 10-20, lakini takriban spishi zote ni ndogo au ndogo sana: spishi ndogo kabisa ina mm 0.05. Utitiri ni tele katika udongo ambapo husaidia kumeng'enya dutu ya viumbehai. Lakini spishi zinazojulikana zaidi ni vidusia vya nje vya wanyama na mimea. Mifano ya vidusia ni kupe, papasi, funduku na utitiri mwekundu.

Kwa kiasili mwili wa matitiri uligawanywa katika sehemu mbili zenye pingili, kama arakinida wengine: prosoma (kefalotoraksi) na opisthosoma (fumbatio). Walakini dalili dhaifu sana za pingili zinabaki katika matitiri. Prosoma na opisthosoma zimeungana na mahali pa ganda kinamo (bopo llinalozunguka kichwa) hutenganisha kelisera na pedipalpi kutoka mwili. Sehemu hii ya mbele ya mwili huitwa gnathosoma. Sehemu iliyobaki ya mwili huitwa idiosoma na ni ya kipekee katika matitiri.

Matitiri wapevu wengi wana jozi nne za miguu, lakini wengine wana michache zaidi. Kwa mfano, matitiri-kinundu, kama Phyllocoptes variabilis (familia Eriophyidae), wana mwili kama mnyoo wenye jozi mbili tu za miguu. Baadhi ya matitiri vidusia wana jozi moja au tatu za miguu katika hatua ya mpevu. Hatua za lava hazina zaidi ya jozi tatu za miguu. Matitiri wapevu walio na jozi tatu tu za miguu wanaweza kuitwa “larviform” (umbo la lava). Pia, wana wa Nematalycidae ndani ya Endeostigmata, ambao huishi kati ya chembe za mchanga, mara nyingi huwa na miili iliyorefuka kama minyoo yenye miguu michache.

Sehemu za kinywa za matitiri zinaweza kutoholewa kwa kung'ata, kudunga, kukeketa au kufyonza. Wanapumua kupitia spirakulo, trakea, matumbo na ngozi yenyewe. Spishi zinazowinda matitiri wengine zina hisi nyepesi, lakini matitiri wengi hawana macho. Macho ya katikati ya arakinida hayapatikani au huungana katika jicho moja. Kwa hivyo, idadi yoyote ya macho kutoka moja hadi matano inaweza kutokea.

Spishi zilizochaguliwa za Afrika

[hariri | hariri chanzo]