Yohane wa Kapestrano

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Yohane wa Kapestrano alizaliwa tarehe 24 Juni, 1386 katika kijiji kinachoitwa kwa Kiitalia Capestrano (wilaya ya L'Aquila), akafa Ilok (katika Korasia ya leo) tarehe 23 Oktoba, 1456.

Alikuwa padri wa Kanisa Katoliki na mtawa wa shirika la Ndugu Wadogo ambalo alichangia kulirekebisha kufuatana na nia za mwanzilishi, Fransisko wa Asizi.

Anaheshimiwa na Kanisa hilo kama mtakatifu na msimamizi wa mapadri wanaohudumia wanajeshi.

[hariri] Maisha

Alisomea Perugia alipopata digrii za sheria ya nchi na ya Kanisa.

Baada ya kupata umaarufu kama wakili, alichaguliwa kuwa gavana wa mji huo hadi ulipotekwa na ukoo wa Malatesta ambao walimfunga.

Gerezani aliongoka, akakubaliwa ndoa yake itangazwe ni batili akaingia utawani kwa Wafransisko.

Kama padri alihubiri katika sehemu kubwa ya Ulaya, hasa upande wa Kaskazini na Mashariki, na kwa namna ya pekee Hungaria.

Lengo la hotuba na kazi zake zote lilikuwa kurekebisha maisha ya Wakatoliki, kupambana na uzushi (hasa Fraticelli, Wajesuati na Wahusi) pamoja na kuwafanya Wayahudi wamuamini Yesu Kristo.

Mwaka 1456 aliagizwa na Papa, akahubri pamoja na ndugu wengine Vita vitakatifu dhidi ya Waturuki waliovamia Ulaya Kusini Mashariki.

Akizunguka Ulaya Mashariki alifaulu kukusanya maelfu ya waamini aliowaongoza kulinda mji wa Beograd (Serbia) mwezi Julai mwaka huo: jeshi la Uturuki lilikimbia na sultani mwenyewe (Mohamed II alijeruhiwa.

Alitangazwa kuwa mtakatifu na Papa Aleksanda VIII tarehe16 Oktoba mwaka 1690.

Vifaa binafsi
Maeneo ya wiki

Vibadala
Vitendo
Urambazaji
Vifaa
Lugha zingine